Browsing: Video Mpya

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amewataka Wazanzibari kuuthamini, kuudumisha na kuenzi Utamaduni wao ikiwa ni pamoja na kuutangaza ndani na nje ya nchi.

Mama Samia ameyasema hayo katika siku maalumu ya sherehe za wakazi wa Kizimkazi iliyopo Kusini Unguja ambapo pia amewataka wazazi kuwachunga vijana wao kutojiingiza katika matumizi ya mihadarati.