Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameshiriki hafla ya kilele cha Jubilee ya miaka 75 ya Shirika la Masista wa Maria Mtakatifu, Malkia wa Afrika iliyofanyika katika Kanisa kuu Jimbo la Sumbawanga leo tarehe 9 Disemba, 2024.
Dkt. Tulia amewasihi Viongozi wa dini pamoja na waumini kuendelea kuliombea amani taifa pamoja na Viongozi wa Serikali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kutekeleza majukumu yake kwa nguvu na afya tele kwa ajili ya Watanzania wote.