Author: Mbeya Yetu

# Ni Madaktari Bingwa wa Samia
#Kwenda Kujifunza hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya

Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya, imeendelea kushiriki katika kukuza na kuimarisha ubora wa huduma za afya nchini na kitovu cha huduma za afya katika Nyanda za Juu Kusini kuwa na madaktari bingwa na bobezi, vifaa tiba vya kisasa katika kuwahudumia wananchi.
Timu ya Viongozi na Wataalamu kutoka Kituo cha afya cha Mt. Theresia Wenda Iringa vijijini ikiongozwa na Mganga Mfawidhi na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani Sr. Dkt. Sabina Mangi, wamefanya ziara ya siku moja katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa lengo la kujionea na kujifunza mambo mbalimbali ya utoaji huduma na pia kuanzisha ushirikiano na Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya kwaajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa kituo hicho cha afya.

Sista Mangi ameeleza kuwa msukumo huwo wa kuitembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya umetokanana na Madakati bingwa na bobezi kutoka hospitali ya kanda Mbeya waliokua wakitoa huduma mkoba ya Madaktari wa Samia katika kituo hicho kuonekana ni watumishi ambao namna wanavyofanya kazi zao kwa furaha, ukamilifu na kwa taaluma hivyo, wakaona ni vyema kuja kujifunza kutoka na ufanisi huo mkubwa walioonyesha

“Tumefika hapa tumeona kweli ni hospitali ambayo watumishi wake wanaonekana ni wanafuraha, wanaonekana wananmwamko, wanaonyesha ownership ya hospitali,na Mkurugenzi ametupokea vizuri akatueleza siri za mafanikio hayo na jinsi wanavyofanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na watumishi. ” – Sr. Mangi
Amesema kupitia ziara hiyo kuwa wamejifunza mambo mnegi ikiwemo kufanya kazi kama timu na ushirikiano, maswala ya ubora kwa utekelezaji wa 5s KAIZEN na ushirikiano mkubwa kati ya Uongozi na watumishi kwa kuishi kama familia na kwa pamoja.

Sr. Mangi ameeleza kuwa na dhamira ya kushirikia na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya katika kuwa na huduma mkoba pia kuanzisha programu ya kubadilishana wataalamu kwenda kituo cha afya cha Mt. Theresia na wengine kuja MZRH kwa lengo la kujengewa uwezo na kujifunza

“Tunataka kufanye kazi na ushirikiano na Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya kwa kuwa na huduma mkoba kila baada ya miezi 3, pili kwapata watumishi watakaokuja kufanya kazi pamoja na sisi kwaajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa kituo chetu, tatu kuwaleta watumishi wetu hospitali ya rufaa ya kanda Mbeya kwaajili ya kujifunza na kujengewa uwezo ili wakirudi waje watujengee uwezo wale hatukupata nafasi ya kuja huku”. – Sr. Mangi

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji, ameupongeza Uongozi wa kituo cha afya cha Mt. Theresia kwa kuichagua Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kamakituo cha mafunzo kwao na kuamua kushirikiana katika nyanja mbalimbali za kutolea huduma za afya kwa wananchi na kuwasihi kufanya kazi kwa furaha na amani ili jamii inapowakuja kupata huduma wanapokea uponyaji haraka hata kabla ya matibabu.

Nae Jofrey Ngumba Muuguzi Mfawidhi wa kituo cha Afya cha Mt. Theresia ameushukru Uongozi wa hospitali ya rufaa ya kanda Mbeya kwa mapokezi mazuri na kupongeza ushirikia ambao wamejifunza kutokana na ziara yao kuwa ya mafanikio.

Read More

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 24 Mei 2024, ametembelea Kanisa la Mtakatifu Bikira Maria lililopo Cairo nchini Misri, eneo ambalo Bikira Maria alijificha na Mtoto Yesu kufuatia tishio la Mfalme Herode kutaka kumuua Mtoto Yesu. Ziara hii inasisitiza umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuendeleza amani, umoja na kuwa na uelewa wa pamoja katika imani na utamaduni wetu.

Read More

Kuelekea Kilele cha siku ya maadhimisho ya Tiba ya magonjwa ya Dharura, wataalamu wa Afya kutoka Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya leo tarehe 24 mei, 2024 wamekutana na kikosi cha Jeshi la zimamoto na uokoaji, Madereva Bajaji na Bodaboda lengo ikiwa ni kutoa elimu juu ya kukabiliana na wagonjwa wa dharura wawapo katika maeneo yao ya kazi.

Akiongea kwa niaba na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Mkurugenzi wa Tiba hospitalini hapa Dkt. Uwesu Mchepange amesema makundi hayo waliyoyachagua ni muhimu sana kwa kuwa hospitali ni kituo cha mwisho cha kupokea wagonjwa wa dharura hivyo ni vema kupeleka elimu pia kwa makundi ambayo yanahusika kwa mara ya kwanza pindi mgonjwa anapopata dharura.

Read More

Baadhi ya Wafanyabiashara wa Maduka Mwanjelwa Kata Ruanda na Kabwe Kata ya Iyela Jijini Mbeya wamefunga maduka yao kwa kile walichodai kunyanyaswa na watumishi wa Mamlaka ya Mapato(TRA)Mkoa wa Mbeya.

Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wafanyabiashara na wanunuzi nje ya maduka wamesema hupata usumbufu kutoka kwa wafanyakazi wa TRA.

Kwa upande wake Musibu Shaban Meneja Mamlaka ya Mapato(TRA)Mkoa wa Mbeya amesema wao kama Mamlaka wanatekeleza majukumu yao zaidi wakidai baadhi ya wafanyabiashara hutoa stakabadhi kinyume na malipo.

Hivi karibuni akiwa Mbeya Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji amepokea malalamiko na kuagiza malalamiko hayo yafanyiwe kazi.

Mgomo huo wa wafanyabiashara umeleta usumbufu mkubwa kwa wateja wanaotoka nje ya Mkoa na nje ya nchi ambao wengi wao hupata mahitaji yao maduka ya Mwanjelwa na Kabwe.

Read More

Halmashauri ya Jiji la Mbeya imezitaka kampuni ya ujenzi ya Cico inayojenga jengo na barabara za mradi wa Tactic na Kampuni ya Mhandisi ambayo ni mkandarasi mshauri kwenye miradi hiyo kuwaondoa wasimamizi wake kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Akizungumza baada ya ziara ya kukagua ujenzi wa barabara za Kalobe-Itende, Machinjioni- Mapelele, Kabwe-Sido na Iziwa, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mhe.Dormohamed Issa amesema, hajaridhishwa na anapata wasiwasi na kasi ya maendeleo ya mradi na hana uhakika kama mkandarasi atamaliza mradi kwa wakati uliopangwa kwa mujibu wa mkataba.

Mstahiki Meya ameongeza kuwa tangu mkandarasi wa kampuni ya Cico alipokabidhiwa na kuanza kazi Novemba, 2023 hakuna alichokifanya kwenye barabara zote, hali ambayo inasababisha wananchi kuendelea kukabiliwa na changamoto ya barabara wakati Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, imeshatoa fedha, hivyo amemtaka mkandarasi kumuondoa Meneja Mradi Mhandisi Bw.Penfeng Wang na Kampuni ya Mhandisi ambayo ni Mkandarasi Mshauri, Bw.Jofrey Kanjanja kwa kushindwa kusimamia kasi ya mradi kama ilivyopangwa.

Read More

Halmashauri ya Jiji la Mbeya imezitaka kampuni ya ujenzi ya Cico inayojenga jengo na barabara za mradi wa Tactic na Kampuni ya Mhandisi ambayo ni mkandarasi mshauri kwenye miradi hiyo kuwaondoa wasimamizi wake kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Akizungumza baada ya ziara ya kukagua ujenzi wa barabara za Kalobe-Itende, Machinjioni- Mapelele, Kabwe-Sido na Iziwa, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mhe.Dormohamed Issa amesema, hajaridhishwa na anapata wasiwasi na kasi ya maendeleo ya mradi na hana uhakika kama mkandarasi atamaliza mradi kwa wakati uliopangwa kwa mujibu wa mkataba. Mstahiki Meya ameongeza kuwa tangu mkandarasi wa kampuni ya Cico…

Read More