Baadhi ya watendaji ngazi ya Kata na kijiji Tarafa ya Ilongo wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya wamekuwa wakilalamikiwa na wananchi kwa kutokutekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwemo kutokusoma taarifa ya mapato na matumizi ya kila baada ya miezi mitatu.Hayo yamebainishwa na afisa tarafa hiyo Bi Magdalena Sikwese alipokuwa kwenye kikao cha kiutendaji amesema amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakilalamikia baadhi ya watendaji hawaweki wazi mapato ya vijiji kwa kuitisha mikutano na kueleza mapato yametumikaje.
Watendaji wa vijiji tunalala kwenye Maeneo yetu,tunasahau wajibu wetu wa kusoma Mapato na matumizi mpaka Wananchi wanalalamika sana mnatakiwa msome Mapato na matumizi Yani tekelezeni majukumu yenu ipasavyo ili kuamsha Hali kwa wananchi kuchangamkia fursa za kuleta maendeleo ya vijiji.”
Baadhi ya watendaji ngazi ya Kata na kijiji Tarafa ya Ilongo wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya wamekuwa wakilalamikiwa na wananchi kwa kutokutekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwemo kutokusoma taarifa ya mapato na matumizi ya kila baada ya miezi mitatu.
Hayo yamebainishwa na afisa tarafa hiyo Bi Magdalena Sikwese alipokuwa kwenye kikao cha kiutendaji amesema amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakilalamikia baadhi ya watendaji hawaweki wazi mapato ya vijiji kwa kuitisha mikutano na kueleza mapato yametumikaje.
Bi Magdalena amesema baadhi ya watumishi wakifika Maeneo Yao ya kazi hasa vijijini wanajisahau kama ni watumishi na kuanza kufanya kazi kwa mazoea kulingana na mazingira
“Watendaji wa vijiji tunalala kwenye Maeneo yetu,tunasahau wajibu wetu wa kusoma Mapato na matumizi mpaka Wananchi wanalalamika sana mnatakiwa msome Mapato na matumizi Yani tekelezeni majukumu yenu ipasavyo ili kuamsha Hali kwa wananchi kuchangamkia fursa za kuleta maendeleo ya vijiji.”
Katika hatua nyingine afisa Tarafa huyo amewakumbusha watendaji kuwa wapo kwenye vijiji na Kata kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania ,hivyo wanapaswa kuwajibika ili ifikapo mwaka 2025 wa uchaguzi aliyewapa dhamana aweze kushindwa kwa kishindo baada ya wananchi kuridhika na utendaji wao kazi.
‘tutimize wajibu wetu Ili mwaka 2025 aliyetutuma tumuwakilishe na tumsaidie kazi kwa wananchi aweze kushindwla kwa kishindo,tutatue kero za wananchi ,tusome Mapato na matumizi na mikutano ya hadharani ifanyike mara kwa mara.
Baadhi ya wananchi wameiomba serikali kutoa muongozo wa matumizi ya mapato ya vijijini ili kuweza kudhibiti ubadhirifu.
“Emmanuel mwaisabila amesema maendeleo ya Kijiji hayawezi kuja kama viongozi wetu hawatokuwa na utaratibu wa kusoma Mapato na matumizi,hivyo tunawaomba wajenge utaratibu wa kutoa taarifa za Mapato na matumizi pamoja na miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Maeneo yetu.
Kwa upande wao baadhi ya watendaji baada ya kikao cha kiutendaji kazi wameahidi kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na kutekeleza majukumu yao kwa weredi.
“Sophia Bernad mtendaji Kata ya utengule Usangu amesema Tutakwenda kutimiza wajibu wetu na kufanya kazi kwa bidii, kutatua kero ya mtu mmoja mmoja na kubuni miradi mbalimbali itakayokwemda kuleta maendeleo kwenye Maeneo yetu ya kazi.