Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila amesema Wilaya ya Mbarali yenye wakazi zaidi ya laki nne na mifugo zaidi ya laki mbili kwa sasa mgogoro mkubwa katika Wilaya yake ni wakulima na wafugaji hasa baada ya mifugo mingi kuondoshwa katika hifadhi ya Ruaha ambako ndiko ilikuwa sehemu ya malisho yao.Baadhi ya Wakulima wa Kijiji cha Mbuyuni Kata ya Mapogolo Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamepigwa na wafugaji baada ya wafugaji hao kuadhibiwa na ofisi ya Kijiji kutokana na kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima. Kwa upande wake Kazi Mwakasala Mwenyekiti wa wafugaji Kata ya Mapogolo amekiri kuwepo kwa migogoro baina ya wakulima na wafugaji ambapo mara kadhaa amepokea malalamiko kutoka kwa wakulima na amekuwa akifanya vikao vya mara kwa mara na wafugaji.
Baadhi ya Wakulima wa Kijiji cha Mbuyuni Kata ya Mapogolo Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamepigwa na wafugaji baada ya wafugaji hao kuadhibiwa na ofisi ya Kijiji kutokana na kuingiza mifugo kwenye mashamba ya wakulima.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wakulima hao wamedai wafugaji wamekuwa wakiingiza maksudi mifugo kwenye mashamba ya wakulima hali inayowafanya wakulima kuwa hatarini kukumbwa na njaa licha ya mazao yao kustawi vizuri.
Maria Ngajilo mkazi wa Mbuyuni amesema yeye ana wagonjwa wanne nyumbani kwake ambao wanategemea chakula hicho lakini wafugaji hao wameingiza mifugo shambani hivyo kumfanya aishi mazingira magumu.
Naye Veronica Amiri amedai ulezi wake umeliwa na mifugo na alipojaribu kuitoa wakulima walimtishia kumpiga kwa fimbo ambazo wafugaji walikuwa nazo.
Aidha Sandina Ramadhani amesema shamba lake la alizeti nalo limeliwa na kundi la mifugo na alipokwenda kutoa taarifa ofisi ya Kijiji hakupata kusikilizwa.
Eliah Chatila naye ni miongoni mwa waathirika wa wafugaji hao mbali ya mazao yake kuliwa na mifugo amepata ulemavu wa kidole kutokana na kipigo kutoka kwa wafugaji licha ya kutoa taarifa Polisi lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Chatila amesema alipokuwa akifuatilia suala hilo mahakamani pamoja na matibabu ambayo aligharamia shilingi laki nane akadaiwa kutoa shilingi laki mbili ili kuiondoa kesi mahakamani lakini alitoa shilingi elfu hamsini.
Katika hatua nyingine baadhi ya wachezaji nao wamedai kupigwa na wafugaji hivi karibuni walipokuwa wakicheza mpira uwanja wa Mbuyuni baada ya wafugaji zaidi ya ishirini kuwazingira kwa fimbo uwanjani hapo.
Geaz Onesmo Ngulo mkazi wa Mbuyuni amedai kuvamiwa na wafugaji hao kishwa kurushwa rushwa kichura baada ya wafugaji kutoka ofisi za Kijiji,ambapo Alex Chengula amesema baada ya kupigwa walitoa taarifa ofisi ya Kijiji na Polisi lakini hakuna hatua zozote zilizochukulia kwa wafugaji.
Naye Enock Mwashitete mwakilishi wa wakulima amesema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu ingawa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Kwangula Misana kuulekeza uongozi wa Kijiji na Kata lakini viongozi hao hakuna hatua walizozichukua.
“Tumetenga eneo la malisho Kitongoji cha Mlimani katika matumizi bora ya ardhi lakini eneo hilo halitumiki kama ilivyokusudiwa badala yake wafugaji wanavamia mashamba ya wakulima na kuwapiga”alisema Mwashitete.
Mwashitete amesema kitendo cha Mtendaji Jane Nyudike kufanya kazi katika kituo cha kazi kwa zaidi ya miaka ishirini imekuwa changamoto kwani amekuwa akifanya kazi kwa mazoea ambapo awali alikuwa akiishi kwenye nyumba ya Katibu wa wafugaji hivyo inakuwa ni vigumu kuwasikiliza wakulima pindi wanapoleta malalamiko ofisini.
Kwa upande wake Kazi Mwakasala Mwenyekiti wa wafugaji Kata ya Mapogolo amekiri kuwepo kwa migogoro baina ya wakulima na wafugaji ambapo mara kadhaa amepokea malalamiko kutoka kwa wakulima na amekuwa akifanya vikao vya mara kwa mara na wafugaji.
Mwakasala amesema hivi karibuni amepokea malalamiko kutoka kwa wakulima ambapo wamedai kupigwa na alipofuatilia ofisi ya Kijiji alipata taarifa suala hilo kupelekwa Polisi.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila amesema Wilaya ya Mbarali yenye wakazi zaidi ya laki nne na mifugo zaidi ya laki mbili kwa sasa mgogoro mkubwa katika Wilaya yake ni wakulima na wafugaji hasa baada ya mifugo mingi kuondoshwa katika hifadhi ya Ruaha ambako ndiko ilikuwa sehemu ya malisho yao.
Hata hivyo ameiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wizara ya Kilimo ili kusaidia kuondoa migogoro kutokana na Wilaya ya Mbarali kuwa na mifugo mingi lakini haina hakuna eneo lililotengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo.
Mwila mbali ya kero hiyo amesema kero nyingine ni uvamizi wa wanyama wakali kutoka hifadhi ya Ruaha ambapo wanyama hao hufuata ushoroba kutoka Ruaha kuelekea Mpanga Kipengele,hivi karibuni mwananchi mmoja mkazi wa Igava ameuawa na Simba mwingine amekanyagwa na Tembo amelazwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya akipatiwa matibabu.
Licha ya kuwepo kwa uhuru wa vyombo vya habari baadhi ya watumishi wa Umma bado wanawazuia Waandishi wa Habari kuibua changamoto mbalimbali kama ilivyotokea kwa Polisi Kata ya Mapogolo Sichana Mselemu na Afisa Tarafa ya Rujewa Donald Mwaigombe ambao wanadai Waandishi hawaruhusiwi kufanya kazi bila vibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.