Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

SERIKALI YA TANZANIA KUWAFUTIA HADHI YA UKIMBIZI WAKIMBIZI WANAOISHI NCHINI.

December 7, 2025

MAZISHI YA SAMSON MWAMAKIMBULA

December 6, 2025

Mbinu aliyotumia kupata kazi ya udereva baada ya kusota sana

December 6, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • SERIKALI YA TANZANIA KUWAFUTIA HADHI YA UKIMBIZI WAKIMBIZI WANAOISHI NCHINI.
  • MAZISHI YA SAMSON MWAMAKIMBULA
  • Mbinu aliyotumia kupata kazi ya udereva baada ya kusota sana
  • MHE. SALOME MAKAMBA AIPONGEZA PBPA KWA UTENDAJI KAZI MZURI
  • Hofu yake zilianza kuathiri hata furaha ya ndoa yake
  • MASACHE AWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUSHIKILIA AMANI
  • MH. MASACHE: TUENDELEE KUISIMAMIA MIRADI ILIYOKUWEPO NA KUIBUA MIPYA AWASHUKURU WANA CHUNYA
  • MH. NOAH MWAKISU AAPISHWA RASMI KUWA DIWANI KATA YA ILOMBA
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » WAANDISHI WA HABARI KUANZA KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA TAI-HABARI – MSIGWA
Habari za Kitaifa

WAANDISHI WA HABARI KUANZA KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA TAI-HABARI – MSIGWA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuMay 3, 2025No Comments10 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Na Mwandishi Wetu, JAB

Serikali imesema vitambulisho vya Uandishi wa Habari (Press Card), vitaanza kutolewa wakati wowote baada ya siku saba kuanzia leo Mei 3, 2025 baada ya Waandishi wa Habari kuanza kujisajili rasmi kwenye mfumo wa TAI-Habari.

Mwandishi wa Habari ataanza kujisajili kupitia kiunganishi cha https://taihabari.jab.go.tz kisha kufuata maelekezo yaliyotolewa ili kukamilisha kujaza fomu yake kwenye mfumo huo wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari.

Kauli hiyo imetolewa tarehe 03 Mei, 2025 na Katibu Mkuu wa Wizara Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa, katika Kijiji cha Sayu mkoani Shinyanga wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu masuala mbalimbali ya Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali mkoani humo.

“Tuliwaahidi kwamba tunawaletea Press Card (Vitambulisho vya kidijitali), ninayofuraha kuwajulisha kwamba ‘press card’ hizi za kidijital mchakato umekamilika, ziko tayari kwa matumizi, siku saba kuanzia sasa mtaingia kwenye kiunganishi cha Bodi ya lthibati ya Waandishi wa Habari na utaomba kitambulisho…,” alisema Bw. Gerson Msigwa.

Alisema Mwandishi wa Habari akishajaza taarifa zake sahihi, Bodi itapokea maombi na kuyahakiki na kama yamekidhi vigezo kitambulisho kitachapishwa na kutumwa mahali alipo kupitia Klabu za Waandishi wa Habari katika maeneo yao.

“Ombi langu kwenu Waandishi wa Habari mtambue kitambulisho hiki ni mali ya Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Tanzania…, hivyo ukipewa wewe ndiye utakayewajibika kwa lolote litakalofanyika kwa utambulisho wa kitambulisho hiki, siyo kitambulisho umekiacha huko, mtu amekichukua kaenda kufanya utapeli tutambaini kwa sababu sasa tutakuwa tunaweza kufuatilia kwa kupitia mfumo, tukibaini tutakupata wewe,” alisema Bw. Msigwa na kuongeza;

“Ninachowaomba kitunzeni kama mboni ya jicho, huu ndiyo utambulisho wenu wa kazi, muwe nacho mfukoni, usikiache hovyo hovyo.”

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, Wakili Patrick Kipangula, ili kurahisisha zoezi la kutuma na kupokea Press Card hizo, Waandishi wa Habari wanahimizwa kujisajili kwenye Klabu za Waandishi wa Habari zilizopo maeneo yao.

Wakili Kipangula alisema wakati wa kujisajili Waandishi wa Habari wanapaswa kuweka kwenye mfumo vyeti vilivyo halali na kwamba ikiwa Mwandishi ataweka cheti cha kughushi, Bodi ya Ithibati itachukua hatua kali za kisheria kwa sababu hilo ni kosa la jinai.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

MHE. SALOME MAKAMBA AIPONGEZA PBPA KWA UTENDAJI KAZI MZURI

December 6, 2025

MH. MAHUNDI: Serikali Yaendelea Kuimarisha Mazingira Wezeshi kwa Biashara za Wanawake Dodoma

November 28, 2025

MIKOPO IWE CHACHU YA KUKUA KIUCHUMI NA KUZITUNZA FAMILIA ZENU – MHE. MARYPRISCA

November 28, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025246

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025234

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024206

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025128
Don't Miss
Video Mpya

SERIKALI YA TANZANIA KUWAFUTIA HADHI YA UKIMBIZI WAKIMBIZI WANAOISHI NCHINI.

By Mbeya YetuDecember 7, 20253

SERIKALI YA TANZANIA KUWAFUTIA HADHI YA UKIMBIZI WAKIMBIZI WANAOISHI NCHINI.

Serikali ya Tanzania imesema inaenda kuwafutia hadhi ya ukimbizi Wakimbizi wanaoishi nchini baada ya kurejea kwa hali ya amani katika nchi zao baada ya hapo awali kuwepo kwa machafuko.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene huku jumla ya Wakimbizi 238,956 wanahifadhiwa hapa nchini ambapo Warundi ni 152,019,Wakongo ni 86,256 na mataifa mengine yakichangia idadi ya 681.

“Katika mkutano wa mwisho tulikubaliana kurejesha Wakimbizi 3000 kwa wiki,hata hivyo hadi tunakutana hapa hii leo 2025 ni Wakimbizi 3000 pekee waliorejea nchini kwao.Hili ni jambo ambalo lingepaswa kukamilika ndani ya wiki moja lakini limechukua takribani mwaka mzima,hatuwezi kuruhusu Hali hii iendelee hivi.” Alisema Waziri Simbachawene

MAZISHI YA SAMSON MWAMAKIMBULA

December 6, 2025

Mbinu aliyotumia kupata kazi ya udereva baada ya kusota sana

December 6, 2025

MHE. SALOME MAKAMBA AIPONGEZA PBPA KWA UTENDAJI KAZI MZURI

December 6, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

SERIKALI YA TANZANIA KUWAFUTIA HADHI YA UKIMBIZI WAKIMBIZI WANAOISHI NCHINI.

December 7, 2025

MAZISHI YA SAMSON MWAMAKIMBULA

December 6, 2025

Mbinu aliyotumia kupata kazi ya udereva baada ya kusota sana

December 6, 2025
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025246

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025234

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024206
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.