wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar akizungumza wakati alipotembelea mafunzo ya Maafisa Waandikishaji
Wasaidizi ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida leo Septemba
19, 2024 katika Shule ya Sekondari Mwenge Mkoani Singida. Mkoa wa Singida na
Dodoma wanataraji kuanza uboreshaji septemba 25 hadi Oktoba mosi mwaka huu.
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar akizungumza wakati alipotembelea mafunzo ya Maafisa Waandikishaji
Wasaidizi ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida leo Septemba
19, 2024 katika Shule ya Sekondari Mwenge Mkoani Singida. Mkoa wa Singida na
Dodoma wanataraji kuanza uboreshaji septemba 25 hadi Oktoba mosi mwaka huu. Katikati
ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bi. Joanfaith Kataraia na kulia ni Afisa
Mwandikishaji Jimbo la Singida Mjini,
Bw. Edward Mboya.
Zakia Mohamed Abubakar ametembelea mafunzo ya Waandishi Wasaidizi ngazi ya
Kata watakao husika na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida na Singida Vijijini mkoani Singida na kuzungumza nao
wakati wa mafunzo yao ya siku mbili yaliyomalizika leo Septemba 19, 2024.
Kata, Dkt Zakia aliwataka kuzingatia mafunzo hayo ili nao waende kuwafundisha
wachini yao lakini kubwa ni kuhusu dhamana waliyopewa ya kuendesha zoezi la
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika maeneo yao.Dkt Zakia amesema umakini mkubwa unahitajika
wakati wa utekelezaji wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura kwani daftari hilo ni nyenzo muhimu
kwa ajili ya Uchaguzi.Aidha amewataka kusoma vyema nyaraka walizopatiwa
ili kuwa na uelewa mpana utakaowawezesha kutatua changamoto zitakazojitokeza wakati
wakutekeleza wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani
Singida.
“Daftari la wapiga kura ni instrument muhimu sana kwa ajili ya
uchaguzi zingatieni mafunzo ili muweze kusimamia uandikishaji wa wananchi na
kuboresha vyema taarifa kwa wale wanaoboresha,” amesisitiza Dkt Zakia.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida,
Joanfaith Kataraia, amemhakikishia mjumbe huyo wa Tume kuwa washiriki wako
makini na wana utayari wa kwenda kutekeleza majukumu yao.
Kataraia amewasisitiza washiriki wa mafunzo
kushirikisha wataalamu wa Tume waliopo katika ukumbi wa mafunzo changamoto
wanazokutana nazo kulingana na mafunzo waliyopewa kabla ya kumaliza mafunzo ili
kuwawezesha kuwa na uelewa wa pamoja.
Mafunzo hayo kwa maafisa waandikishaji ngazi ya Kata
yamefanyika kwa siku mbili kuanzia Septemba 18-19, 2024.
Maafisa waandikishaji wasaidizi Ngazi ya Kata
kutoka Kata zote za mkoa wa Singida wamepatiwa mafunzo ya utumiaji wa Mashine
za BVR pamoja na ujazaji wa fomu mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji
wa Dafrati la Kudumu la Wapiga Kura unaoitaraji kuanza Septemba 25 2024 hadi Oktoba 1 mwaka huu.
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar (wapili
kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bi. Joanfaith Kataraia (kulia)
wakiangalia mafunzo kwa vitendo yaliyokuwa yakifanywa na Maafisa Waandikishaji
Wasaidizi Ngazi ya Kata wakati alipotembelea mafunzo yao leo Septemba 19, 2024
katika Shule ya Sekondari Mwenge Mkoani Singida. Mkoa wa Singida na Dodoma
wanataraji kuanza uboreshaji septemba 25 hadi Oktoba mosi mwaka huu.