wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari
akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa Wadau wa Uchaguzi katika kisiwa cha
Unguja, Zanzibar leo Septemba 30, 2024 ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
imekutana na wadau mbalimbali wa uchaguzi kuwapa taarifa juu ya uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaotaraji kufanyika Visiwani Zanzibar kuanzia
Oktoba 7 hadi 13, mwaka huu.

Kura Zanzibar utafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 07 hadi 13 Oktoba, 2024
ambapo vituo vitafunguliwa saa 02:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.Akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi
Kisiwani Pemba, Zanzibar, Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,
Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk amesema uboreshaji
huo wa daftari utajumuisha mikoa ya Mjini Magharibi, Unguja Kaskazini, Unguja
Kusini, Pemba Kaskazini na Pemba Kusini.
unafanyika kwenye mzunguko wa sita kwa mujibu wa kalenda ya Tume kwa upande wa
Zanzibar utahusu kuwaandikisha watanzania wote wanaoishi Zanzibar ambao wanastahili
kuandikishwa kuwa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano.Akizungumza wakati akifungua mkutano kama huo
Kisiwani Unguja, Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ambaye pia ni Jaji wa
Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari ameongeza kuwa kwa kuzingatia masharti ya
kifungu cha 13(2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na.1 ya
Mwaka 2024, Tume itawaandikisha watanzania waliopo Zanzibar ambao wametimiza umri
wa miaka 18 na zaidi au watakaotimiza umri huo wakati au kabla ya tarehe ya
uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Amefafanua kuwa mtanzania huyo
atakeyandikishwa ni lazima awe hajapoteza sifa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi
au sheria nyingine yeyote na awe anastahili kuandikishwa kuwa mpiga kura kwa
ajili ya uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
“Kwa lugha nyepesi ni kwamba, Tume
itamwandikisha mtanzania yeyote aliyopo Zanzibar ambaye amekosa sifa za
kuandikishwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC). Hivyo, atakayeandikishwa
kwenye Daftari la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi atapiga kura moja tu ya
kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Jaji Asina.
Uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari ulifanyika
tarehe 20 Julai, 2024 mkoani Kigoma na mpaka sasa uboreshaji umeshafanyika
kwenye mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara,
Simiyu, Manyara, Singida na sehemu ya mkoa wa Dodoma.
wa uchaguzi kutoka vyama vya Siasa, Makundi maalum ya Wanawake, vijana, watu
wenye Ulemavu, Wazee wa Kimila, Wahariri wa vyombo vya Habari wakishiriki
katika mkutano wa Tume na Wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Septemba 30, 2024 katika
kisiwa cha Unguja Zanzibar ikiwa ni maandalizi kuelekea zoezi la uboreshaji wa
daftari la Kudumu la Wapiga Kura visiwani Zanzibar ambalo linataraji kuanza Oktoba
7 hadi 13, mwaka huu.

Wadau wa uchaguzi kutoka vyama vya Siasa, Makundi maalum ya Wanawake, vijana, watu wenye Ulemavu, Wazee wa Kimila, Wahariri wa vyombo vya Habari wakishiriki katika mkutano wa Tume na Wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Septemba 30, 2024 Kisiwani Zanzibar ikiwa ni maandalizi kuelekea zoezi la uboreshaji wa daftari la Kudumu la Wapiga Kura visiwani Zanzibar ambalo linataraji kuanza Oktoba 7 hadi 13, mwaka huu.