Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi alivyo fika katika Ofisi za wataalamu wa kutengeneza Mfumo wa Jamii namba pamoja na jamii xchange zilizopo Zanziba Leo Tarehe 25 Oktoba , 2024 hii ikiwa ni ufatiliaji wa maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani kwamba ifikapo Mwezi Desemba mifumo yote iwe imesomana,
Aidha , katika ziara yake hiyo Mhe. Mahundi amefurahishwa na Jinsi wataalamu walivyo fikia hatua nzuri ya kuunganisha mifumo yote kusomana , na amewataka wataalamu kutoka Nida, Uhamiamiaji pamoja na Rita kuhakikisha wanashirikiana Ili ifikapo Desemba watanzania wote wawe wanaweza kutumia jamii namba na kuwaondolea usumbufu wa kubeba vitambulisho vingi wanapo kuwa wanahitaji huduma kutoa katika Ofisi mbalimbali.
Kwa upande wake, msimamizi wa mradi wa DTP Bw. Bakari ambaye pia ndo mratibu wa mradi wa Jamii namba amemueleza Mhe. Mahundi kuwa mpaka sasa hivi mifumo mingi imeshaanza kusomana na amemuhakikishia ifikapo Desemba mwaka huu, mifumo yote ya Taasisi za serikali na zisizo za serikali itakuwa imeshasomana.
#Tanzania ya KidijitaliInawezekana#