Kizaazaa kilizuka katika kijiji kimoja baada ya mwanamke mzima kufumaniwa akimfanyia uchawi binti yake wa kwanza, lengo likiwa kumzuia asiolewe na kuondoka nyumbani. Tukio hilo liligeuka gumzo mitaani huku majirani wakishindwa kuamini kwamba mama mzazi angeweza kumfanyia mtoto wake kitendo cha aina hiyo.
Kwa muda mrefu, binti huyo mwenye umri wa miaka 26 alikuwa akilalamika kuwa kila uchumba wake unavunjika ghafla bila sababu za maana. Wachumba walikuwa wakimposa kwa furaha lakini kabla harusi haijafika, kila mmoja aliishia kumpiga kisogo.
Familia ilianza kudhani pengine ni tabia yake au bahati mbaya, lakini hali ilipojirudia mara kwa mara, maswali yakaibuka.
Siku ya kufumaniwa, mama huyo alinaswa na ndugu wa karibu wakiwa wamemfuatilia kwa muda mrefu. Walidai walimwona usiku wa manane akifanya tambiko nyuma ya nyumba huku akitaja jina la binti yake.
Baadhi ya vitu vya ajabu vilivyokutwa ni pamoja na nywele, nguo za ndani za binti huyo na kinyesi cha ndege waliodaiwa kuchukuliwa makusudi. Ndipo mshangao mkubwa ulipotanda kwa familia nzima. Soma zaidi hapa