Wakuu wa idara Sekta ya Afya wametakiwa kujenga tabia ya kuwafahamu kwa undani watu wanaowaongoza ili kujiepiusha na migongano mbalimbali inayoweza kuathiri utendaji kazi katika maeneo yao kazi.
Hayo yamesemwa leo tarehe 13 disemba, 2024 na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wakati akihitimisha kikao kazi cha Siku 2 cha kufanya tathimini ya kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa njia bora za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na mtoto kwa kanda ya Nyanda za juu kusini magharibi kwa mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa.
“…hakikisheni mnawafahamu watu mnaowaongoza vizuri na usiruhusu kupambana na mtu, jitahidi upate kibali kwao kitakachokupelekea wakuunge mkono”. – Dkt. Mbwanji
Aidha amewataka watumishi kuto tenganisha furaha na kazi kwa kuwa ni muhimu kufanya hivyo hasa kwa kuwapa nafasi watu wanaowaongoza kwani ni njia bora ya kupunguza msongo wa mawazo itakayopelekea kuongezeka kwa hamasa katika utekelezaji wa majukumu yao wawapo maeneo yao ya kazi.
“…kosa tunalofanya watumishi na viongozi wenzangu ni kutenganisha furaha ya maisha yetu na kazi, niwaombe muda sahihi wa kuwa na furaha ni sasa”. – Dkt. Mbwanji
Akiongea kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Lighton Alex amewataka washiriki wa kikoa kazi hicho kuhakikisha mambo yote taliyojadiliwa katika kikao hicho yanatekelezwa kwa kuwa kwasasa serikali haidaiwi kitu zaidi ya huduma bora kutoka kwa watumishi hao.
“…viongozi wote tuna jukumu kubwa sana la kuhakikisha yale yaliyojadiliwa katika kikao hiki yanatekelezwa’. – Dkt. Lighton Alex
Kwa upande wake Afisa mradi kutoka Idara ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto Joachim Masunga amewaasa watumishi hao kuwa na ushirikiano katika maeneo mbalimbali hasa eneo la takwimu ili kupata takwimu sahihi za mkoa zitakazo pelekea urahsi katika utekelezaji wa majukumu yao.
“… nendeni mkashirikiane kwenye maeneo yote hasa kwenye eneo la takwimu kwa kuwa takwimu za mkoa ni za kwenu wote’. – Joachim Masunga
Magdalena Swebe ni mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi akishukuru kwa niaba ya viongozi mbalimbali waliohudhuria kikao hicho ameahidi yale yote yaliyojadiliwa yataenda kutekelezwa ili kuwa mfano kwa watumishi wa chini wanaowaongoza.