Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na Shirika la CARE wametoa mafunzo kwa wawezeshaji wa ngazi ya jamii kuhusu mabadiliko ya tabia nchi mkoani Mbeya kupitia Mradi wa Ustahimilivu Wake, Dunia Yetu unaotekelezwa katika vijiji 300 vya Mbeya, Njombe na Iringa.
Mafunzo hayo ya siku tatu yamefanyika kijiji cha Chimala, wilayani Mbarali, yakilenga kuwajengea wakulima na wafugaji uelewa wa masuala ya jinsia, utunzaji wa mazingira na mbinu za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

