Serikali mkoani Rukwa imekiri kuwepo uzembe katika usimamizi na ufuatiliaji wa ujenzi wa Vituo vya Afya Viwili na Hospitali ya Manispaa ya Sumbawanga,Mkoani Rukwa, yenye gharama ya shilingi Bilioni 2.6 ambayo imeshindwa kukamilika kama ilivyopanga lakini fedha zote zimekwisha.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa QUEEN SENDIGA ameendelea na ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya ujenzi wa miundombinu ya sekta ya afya, katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, ambapo imebainika matumizi ya fedha hayalingani na thamani ya fedha iliyotengwa na serikali.
Sendiga amesema mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mollo kilichotengewa shilingi Milioni 400 fedha zimekwisha majengo matano hayajakamilika, Kituo cha Afya cha Matanga kilichopelekewa shilingi Milioni 500 fedha zimeisha majengo hayajakamilika, Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Sumbawanga yua ISOFU iliyotumia shilingi Bilioni 1.8 majengo yake hayajakamilika.
Amesema kuna uzembe ambao umetumika kutekeleza miradi hiyo, na uzembe umejitoikeza katika usimamizi na ufuatiliaji, kwani utekelezaji wa miradi yote hiyo inakwenda kwa mfumo wa Force akaunti, Wananchi hawashirikishi katika utekelezaji wa miradi.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga SEBASTIAN WARYUBA naye amekiri watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga wamemuangusha kwasababu uzembe huo unawahusu, ikiwemo idara ya uhandisi, idara ya manunuzi na watendaji wengine.
Hata hivyo Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dokta IBRAHIMU ISAACK amebaini ukikwaji wa miongozo ya utekelezaji wa mfumo wa Force akaunti, ambapo ofisi ya manunuzi katika ofisi ya mkurugenzi iliwanunulia vifaa wananchi badala ya wajumbe wa kamati ya ujenzi wa vituo vya afya.
*********************MWISHO*******************
Trending
- Serikali Kutoa Mafunzo Maalum kwa Waandishi wa Blogu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
- ONYO KALI KWA VIBAKA KUTOKA KWA WAMACHINGA SOKO LA JIONI KABWE JIJI LA MBEYA VIBAKA NA WEZI WAUFYATA
- MNEC: MWASELELA ASIMAMISHA MINONG’ONO YA KISIASA MBEYA MJINI
- KWA MARA NYINGINE, MHANDISI MAHUNDI AWAPA NEEMA WAGONJWA WA MACHO
- MWAKIPESILE AREJESHA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI
- Msimu wa pili wa tamasha la michezo na vipaji MZRH
- MKULIMA NA MFUGAJI WA MBARALI ATIA TIMU KIPUTE JIMBO LA MBARALI USANGU ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE
- WAKILI MSOMI KAPTENI MSTAAFU SAMBWEE SHITAMBALA ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA MBEYA MJINI.