Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 2 Machi, 2024 ameshiriki katika Jopo la kujadili “Jukumu la Mabunge katika kuendeleza amani na maendeleo Duniani” ambalo ni sehemu ya Mkutano wa Kidiplomasia wa Antalya ulioanza jana tarehe 1 Machi 2024 kwa kufunguliwa na Mhe. Recep Tayyip Erdogan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki.
Dkt. Tulia aliongoza sehemu ya majadiliano hayo na kuelezea namna Bunge linavyoendelea kuchagiza amani na demokrasia nchini Tanzania pamoja na Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unavyoendelea kutafuta suluhu na amani kwa Wanachama wake wakiwamo Urusi na Ukraine, Israel na Palestina, Azerbaijan na Armenia na wengine ambao wapo katika migogoro ya kukosa amani.
Mkutano huu unatarajiwa kuhitimishwa kesho tarehe 3 Machi, 2024 Jijini Antalya, Uturuki.