Askofu Ludovick Minde, Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi, ateta na walemavu: Katika siku maalum ya Ibada na hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kusali na walemavu kutoka Vikarieti nne za Jimbo, Rombo, Vunjo, Moshi na Hai hapo jana.
Askofu Minde katika mahubiri yake alisema zipo aina mbili za ulemavu na Ulemavu unaoonekana na usioonekana.
Hivyo walemavu wasijione kuwa wao ni tofauti na watu wengine. Watu wote ni sana.
Ameeleza kuwa Ulemavu wao kama wanavyoonekana; sio jambo litakalowanya wajione tofauti na watu wengine. Ni lazima wajiongeze kwa kutokomeza dhana ya utegemezi kwani wakiwezeshwa wanaweza kufanya shughuli za maendeleo katika familia zao.
Askofu Minde ameiasa jamii kutoa ushirikiano kwao na kuwasaidia bila kuchoka pale inapowezekana.
Baadae walishiriki hafla fupi kwa pamoja na kusema zoezi hilo ni endelevu, kila mwezi Septemba kushiriki Ibada na hafla kwa walemavu kijimbo wakristo na wasio wakristo.