Author: Mbeya Yetu

Mama Janeth Magufuli, mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli, akifurahi na wanafunzi nyumbani kwake Chato leo Machi 18, 2023.

Mama Janeth amewaasa wanafunzi wasichana katika Shule za Msingi na sekondari nchini kote kujiepusha kabisa na mambo yanayoweza kuathiri maendeleo yao kimasomo.

Mama Magufuli amesema mambo mengi ya Kisasa hususan ya mitandao yamekuwa yakitengua mawazo chanya ya wasichana, na kuwashawishi waishi maisha ya mtandao ambayo mengi yao si maisha halisi.

“Kwa hiyo binti zango elekezeni akili, maarifa na juhudi katika masomo na sio mambo mengine yanayoweza kuathiri maendeleo yenu kimasomo kama vile mambo ya mitandao ambayo mengi sio yenye kuonesha maisha halisi”, alisema Mama Magufuli leo Machi 18, 2023 nyumbani kwake Chato, Mkoa wa Geita.

Mjane huyo wa Hayati Dkt. Magufuli alikuwa akiongea machache baada ya kutoa misaada ya taulo za wasichana na Baiskeli za magurudumu kwa Shule tatu za Sekondari za Wasichana zilizomo wilayani Chato.

Read More

Ibada maalumu ya kumuombea mwaka wa pili wa kifo chake aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika kanisa la Mt. Yohana Maria Muzeyi Parikoa ya Mlimani, Chato, Geita ikiongozwa na Askofu Mkuu Jimbo la Katoliki la Rulenge, Ngara, leo Ijumaa Machi 17, 2023.

Mjane wa Marehemu, Mama Janeth Magufuli, anaongoza wanafamilia.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Innocent Bashungwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigella, Mjumbe wa NEC CCM Zanzibar upande wa vijana Ndugu Mwanaenzi Suluhu Hassan na viongozi wengine wa mkoa na wilaya wapo kanisani

Read More

Utalii ni shughuli zinazochangia sehemu kubwa katika pato la Taifa. Miongoni mwa mikoa yenye shughuli nyingi za utalii ni pamoja na muikoa ya Nyanda za Juu Kusini kutokana na kuwa na vivutio mblimbali vya Utali, tazama makala haya ili kufahamu avivutio vya utalii vilivyopo kwenye mikoa hiii.

Read More