Baadhi ya wanawake wanafunzi a wananchi wakiwa kwenye Banda la DMI katika Maonesho yaTano ya Elimu Juu Zanzibar.
Makamu Mkuu wa Chuo cha DMI (Taaluma) Dkt.Wilfred Johnson Kileo akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Maonesho ya ya Tano Wiki ya Elimu ya Juu inayofanyika Viwanja vya Maisara Zanzibar
DMI yawaasa Wasichana kujiunga kada ya Ubahari
*Yasema hakuna kizuizi cha kufanya mwanamke kuwa baharia
Na Mwandishi Wetu,Zanzibar
Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimewataka wahitimu wanawake wa kidato cha sita cha mwaka huu kujitokeza kujiunga na kada ya ubaharia katika chuo hicho.
Kauli hiyo ameitoa jana Makamu Mkuu wa Chuo cha DMI (Taaluma) Dkt. Wilfred Johnson Kileo kwenye maonyesho ya tano ya Wiki ya Elimu ya Juu yalinayofanyika viwanja vya Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema DMI inatia moyo kwa wahitimu hao ambao ni wanawake kutokana na kuwa, siku hizi hakuna vizuizi kwao kujiendeleza kwenye taaluma mbalimbali nchini.
Makamu Mkuu wa Chuo cha DMI alisema katika idadi ya wanafunzi ambao wanasoma ya 5,170 wanafunzi 1,300 ni wanawake.
“Tunaona idadi hiyo tayari inawapatia muitikio wanawakae kujiunga kwenye taaluma za bahari hivyo wanatakiwa wasiwe waoga kutokana na
kuwa hizi ni kazi kama kazi zingine,” alisema
Alisema mashirika mengi yanayohusu masuala ya bahari yameweka mambo mengi ya kuwazingatia wanawake katika kutunza haki zao kwenye kazi za meli .
“Kwa kuwa tunaingia kwenye Uchumi wa Buluu lazima wajitokeze kutumia fursa hii kwa kujiunga na DMI ili wapate ujuzi na kwenda kufanyia kazi,” alisema
Alisema kutokana na kuwa serikali inaweka mkazo kwenye eneo la Uchumi wa Buluu hivyo kuna haja ya idadi kubwa ya wanawake kujitokeza kujiunga ili wanufaike na eneo hilo la Uchumi wa Buluu.
“Uchumi wa Buluu bila ya rasilimali watu wenye uweledi hatutaweza kufika azma hiyo hivyo ni wakati kwa wanawake kuja kunufaika na eneo hili la uchumi wa buluu kupitia Elimu na Mafunzo yanayotolewa Chuoni,” alisema