AJALI YA GARI KUGONGA MAGARI MATATU NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI.Ni kwamba mnamo tarehe 16.08.2022 majira ya saa 02:00 asubuhi huko maeneo ya Inyala Pipeline, Kijiji cha Shamwengo, Kata ya Inyala, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya katika barabara ya Mbeya – Njombe, Gari lori lenye namba za usajili T.387 DFJ lenye tela namba T.918 DFE aina ya Dayun likiendeshwa na Dereva MUHSIN GUMBO, Mkazi wa Dar es Salaam mali ya kampuni ya Evarest Frech Ltd likiwa na kontena la mchanga likitokea Mbeya liligonga kwa nyuma Gari T.966 DUQ aina ya Fuso basi mali ya kampuni ya Super Rojas likitokea Mbeya kuelekea Njombe likiendeshwa na ALEX MGIMBA [51] Mkazi wa Jijini Mbeya na kisha kugonga Gari T.836 DRE Mitsubish Benz iliyokuwa ikiendeshwa na NEDIM PREMJI, Mkazi wa Dar es Salaam na kisha kugonga Gari linguine T.342 CHG/T.989 CGS Scania iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika na kusababisha vifo vya watu 19 kati yao wanaume ni 12, wanawake 06 na mtoto 01. Aidha katika ajali hiyo majeruhi ni 10 kati yao wanaume ni 07, wanawake ni 02 na mtoto 01.Chanzo cha ajali ni Gari kufeli breki kwenye eneo lenye mteremko mkali na kisha kugonga magari mengine. Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na Hospitali ya Igawilo. Imetolewa na:Ulrich Matei – SACPKamanda wa Polisi,Mkoa wa Mbeya.
Trending
- Dkt. Tulia Aongoza kwa Vitendo, Apiga Kura na Kuhamasisha Ushindi wa CCM Uyole
- DKT MARY MWANJELWA AUNGANA NA WANANCHI KUPIGA KURA AHAMASISHA KUJITOKEZA KWA WINGI AMANI IMETAWALA
- Nilivyookoa Ndoa Yangu Baada ya Migogoro Kila Usiku Kuhusu Pesa na Wivu
- MWAKIPESILE: ”TUKAANDAMANE OKTOBA 29 KWA AJILI KUWAPIGIA KURA VIONGOZI KWA AMANI”
- “Tunatiki CCM, Tunatunza Amani” — Kauli ya Bodaboda Kiwira Yakonga Moyo wa Suma Fyandomo
- Nilivyomfanya Mtu Aliyenidharau Kuniheshimu na Kunitegemea Kwa Mambo Mengi
- NABII MPANJI AUTANGAZIA UMMA, WAKRISTO WASISHIRIKI MAANDAMANO WAJITOKEZE KWA WINGI KUPIGA KURA
- Nilivyookoa Biashara Yangu Baada ya Wateja Wote Kupotea Ghafla

