Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Kijana Golden Kidumba (DON. G) Awagusa Watoto wa Mitaani kwa Chakula na Mavazi

November 19, 2025

Biashara ya mbao ilivyobadili maisha yake ikimpa utajiri

November 19, 2025

Rais Dkt Samia aongoza kikao kazi cha Mawaziri Naibu Mawaziri Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu

November 19, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Kijana Golden Kidumba (DON. G) Awagusa Watoto wa Mitaani kwa Chakula na Mavazi
  • Biashara ya mbao ilivyobadili maisha yake ikimpa utajiri
  • Rais Dkt Samia aongoza kikao kazi cha Mawaziri Naibu Mawaziri Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu
  • Safari ya kurejesha hamu ya tendo la ndoa kwa Zuhura iliyofanikiwa
  • Kutoka kusota hadi usukani wenye utajiri
  • Ikulu Dodoma: Rais Samia Azungumza na Mawaziri Baada ya Kuwaapisha
  • Alivyokabiliana na changamoto ya ukosefu wa hamu ya tendo hadi kuishinda
  • DKT. MWIGULU AKABIDHIWA OFISI RASMI
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » MH MHANDISI MARYPRISCA MAHUNDI AZINDUA WIKI YA TAFITI NA BUNIFU MUST MBEYA
Video Mpya

MH MHANDISI MARYPRISCA MAHUNDI AZINDUA WIKI YA TAFITI NA BUNIFU MUST MBEYA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuDecember 3, 2024No Comments0 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya amezindua wiki ya utafiti na ubunifu Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya.

Katika hotuba yake Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema tafiti na bunifu ndiyo nguzo kuu ya uchumi Duniani.

Amesema Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kiwe sehemu ya majibu na lazima wanachuo wajitofautishe na kada nyingine kwani soko lipo ndani na nje ya nchi.

Amesema juhudi za tafiti na bunifu Chuo Kikuu MUST kimemfanya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuvutiwa na kutoa pesa kupanua huduma Mkoa wa Rukwa.

Amewahimiza wanachuo kusoma kwa bidii ili kukitangaza Chuo ndani na nje ya nchi huku akisisitiza kauli mbiu “Nafasi ya utafiti na ubunifu katika kuimarisha kilimo” alisema Mahundi.

Amepongeza Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kwa kubuni dira za maji ambazo zinasambazwa nchini huku akihimiza bunifu katika kilimo ili waweze kujiajiri badala ya kutegemea ajira serikalini.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

Kijana Golden Kidumba (DON. G) Awagusa Watoto wa Mitaani kwa Chakula na Mavazi

November 19, 2025

Rais Dkt Samia aongoza kikao kazi cha Mawaziri Naibu Mawaziri Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu

November 19, 2025

Ikulu Dodoma: Rais Samia Azungumza na Mawaziri Baada ya Kuwaapisha

November 18, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025230

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025226

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024200

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025127
Don't Miss
Video Mpya

Kijana Golden Kidumba (DON. G) Awagusa Watoto wa Mitaani kwa Chakula na Mavazi

By Mbeya YetuNovember 19, 20251

Kijana Golden Kidumba, maarufu kama DON. G, amewagusa watoto wa mitaani kwa kuwapatia chakula, kuwanunulia nguo na kutumia muda wa siku nzima akiwa nao, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuikumbuka jamii aliyotokea.

Golden, mzaliwa na mkazi wa zamani wa Njombe, anasema maisha magumu aliyoyapitia utotoni ndiyo yamemfanya kuwa na moyo wa huruma na kujitoa kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

“Nimekulia kwenye maisha magumu sana. Lakini namshukuru Mungu kwa kunibariki na kunifanya niweze kuwakumbuka hawa wadogo zangu wa mitaani. Nimekula nao, nimesherehekea nao na pia nimewanunulia nguo ili wajisikie wanathaminiwa kama watoto wengine,” amesema DON. G.

Amesema kusaidia watoto wa mitaani si tukio la leo pekee, bali ni jambo alilolianza miaka kadhaa iliyopita, ikiwemo kutembelea hospitali na kuwasaidia watu wenye uhitaji.

Golden ameweka wazi kuwa ndoto yake ya baadaye ni kuanzisha taasisi ya msaada na hata kujenga shule maalum kwa ajili ya watoto hao, ili kuwapa elimu, malezi na fursa za kuanza maisha mapya.

Baadhi ya watoto wa mitaani waliopokea msaada huo wameeleza machungu ya maisha yao, ikiwemo vipigo, njaa, manyanyaso na mara nyingi kudharauliwa kama wahalifu bila kujua historia zao.

Kijana Brian Edwin, anayelelewa katika kituo cha Mtama, amesema:
“Maisha ya mitaani ni magumu. Tunapigwa, tunanyanyaswa na tunaishi bila uhakika. Lakini leo tumepata faraja kubwa kutoka kwa DON. G. Mungu ambariki.”

Wengine kama Anody Nyondo na Gifty wameeleza jinsi walivyokimbia nyumbani kutokana na migogoro ya kifamilia na manyanyaso, hali iliyowalazimu kuingia mitaani.

Watoto hao wameiomba jamii na serikali kutowatenga, bali kuwaona kama watoto wanaohitaji msaada na si wahalifu.

Golden ameendelea kutoa wito huo huo:
“Tusishikilie mali bila sababu. Tukiondoka duniani, hatuchukui chochote. Tuwakumbuke watoto wa mitaani; wanahitaji upendo na msaada wetu.”

Biashara ya mbao ilivyobadili maisha yake ikimpa utajiri

November 19, 2025

Rais Dkt Samia aongoza kikao kazi cha Mawaziri Naibu Mawaziri Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu

November 19, 2025

Safari ya kurejesha hamu ya tendo la ndoa kwa Zuhura iliyofanikiwa

November 19, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Kijana Golden Kidumba (DON. G) Awagusa Watoto wa Mitaani kwa Chakula na Mavazi

November 19, 2025

Biashara ya mbao ilivyobadili maisha yake ikimpa utajiri

November 19, 2025

Rais Dkt Samia aongoza kikao kazi cha Mawaziri Naibu Mawaziri Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu

November 19, 2025
Most Popular

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025230

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025226

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024200
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.