Watumishi wa Afya ambao ni Mabalozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kutoka Dodoma jana wamefanya ziara ya mfano kuitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma (DRRH) na kutoa msaada wa vifaa tiba na dawa kwa watoto wanaohitaji huduma za afya.
Akizingumza na Wafanyakazi wa wodi ya Watoto wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Bi. Naima Mkingule ambae ni Kiongozi wa msafara amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za afya, jamii, na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa watoto wanapata huduma bora na kwa haraka.
“Katika kuhakikisha watoto wetu wanapata huduma bora za afya, ni muhimu kuunganisha nguvu zetu. Ushirikiano kati ya taasisi za afya, jamii, na wadau wengine ni msingi wa mafanikio yetu katika kutatua changamoto za kiafya zinazowakabili watoto.” – Bi. Naima Mkingule, Kiongozi wa Msafara.
Mkingule ameeleza kuwa msaada huo wa vifaa tiba na dawa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Wizara ya Afya katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya maeneo mbalimbali nchini, hususan kwa watoto, ambao wanahitaji huduma za matibabu ili kuweza kupona magonjwa yanayoathiri maisha yao.
Trending
- Nilihangaika na Migogoro ya Familia Kwa Miaka Mingi, Lakini Siri Niliyotumia Ikarudisha Upendo na Amani Nyumbani
- Basi tulipolala na mume wangu, kila mtu aligeukia upande wake
- SHIRIKA LA POSTA LATOA ZAWADI ,VYETI KWA WASHINDI WA UANDISHI WA BARUA MBEYA.
- SERIKALI IMEWEKA MIKAKATI DHABITI YA KUKABILIANA NA MAJANGA NCHINI-MAJALIWA
- WIKI YA VIJANA YAPAMBWA NA MPAMBANO, TIMU 8 KUKIPIGA KWENYE BREW MASTER MWENGE NDONDO CUP
- Ilifikia hatua hadi nikawa namuogopa mume wangu kitandani
- MAWAZIRI WAIMWAGIA PONGEZI BENKI YA NMB KWA UTENDAJI WAKE.
- Benki ya NMB yashiriki kwenye ufunguzi wa Wiki ya Vijana inayofanyika Kitaifa Mbeya