Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Nilivyookoa Ndoa Yangu Baada ya Migogoro Kila Usiku Kuhusu Pesa na Wivu

October 27, 2025

MWAKIPESILE: ”TUKAANDAMANE OKTOBA 29 KWA AJILI KUWAPIGIA KURA VIONGOZI KWA AMANI”

October 27, 2025

“Tunatiki CCM, Tunatunza Amani” — Kauli ya Bodaboda Kiwira Yakonga Moyo wa Suma Fyandomo

October 27, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Nilivyookoa Ndoa Yangu Baada ya Migogoro Kila Usiku Kuhusu Pesa na Wivu
  • MWAKIPESILE: ”TUKAANDAMANE OKTOBA 29 KWA AJILI KUWAPIGIA KURA VIONGOZI KWA AMANI”
  • “Tunatiki CCM, Tunatunza Amani” — Kauli ya Bodaboda Kiwira Yakonga Moyo wa Suma Fyandomo
  • Nilivyomfanya Mtu Aliyenidharau Kuniheshimu na Kunitegemea Kwa Mambo Mengi
  • NABII MPANJI AUTANGAZIA UMMA, WAKRISTO WASISHIRIKI MAANDAMANO WAJITOKEZE KWA WINGI KUPIGA KURA
  • Nilivyookoa Biashara Yangu Baada ya Wateja Wote Kupotea Ghafla
  • DED Yegella: Ahamasisha Upigaji Kura, Kamanda Kuzaga Asema Jeshi la Polisi Lipo Tayari Kulinda Amani
  • RC Malisa Atoa Wito wa Kulipa Leseni Wakati Akikabidhi Madawati 1,000 kwa Shule 15 Jijini Mbeya
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » MH. MAHUNDI: SERIKALI YABORESHA MAWASILIANO KATA YA MKWAMBA RUKWA KUPITIA MIRADI YA UCSAF
Habari za Kitaifa

MH. MAHUNDI: SERIKALI YABORESHA MAWASILIANO KATA YA MKWAMBA RUKWA KUPITIA MIRADI YA UCSAF

Mbeya YetuBy Mbeya YetuJune 8, 2025Updated:June 8, 2025No Comments8 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprsca Mahundi, amewatoa hofu wananchi kuwa Serikali inaendelea kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata huduma bora za mawasiliano hasa maeneo ya vijijini.

Katika kutekeleza hilo, kata ya Mkwamba iliyopo mkoani Rukwa yenye jumla ya vijiji vinne—Swaila, Tambaruka, Itindi na Lyele—imepata mafanikio makubwa kupitia miradi ya Serikali inayolenga kuboresha mawasiliano.

Kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Serikali imefanikiwa kujenga minara ya mawasiliano kwa kushirikiana na makampuni ya mawasiliano ya VODACOM na HALOTEL.

Mnara wa Vodacom umejengwa katika Kijiji cha Tambaruka kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali (DTP), huku mnara wa Halotel ukijengwa katika Kijiji cha Itindi chini ya awamu ya tatu ya mradi wa mawasiliano vijijini.

Minara yote imewashwa na inatoa huduma kwa wananchi, hatua inayowezesha kuimarika kwa shughuli za kijamii na kiuchumi kupitia mawasiliano ya uhakika.

Meneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Mkoa wa Rukwa, Bw. Ching’uli, amesema utekelezaji wa miradi ya UCSAF umeleta mabadiliko makubwa katika maisha ya wananchi wa Wilaya ya Nkasi kwa kuwaunganisha na huduma muhimu za mawasiliano.

Amesema kuwa kupitia minara iliyojengwa katika maeneo kama Kala, Izinga na Mlambo, wananchi wameweza kuwasiliana kwa urahisi zaidi, kupata taarifa kwa haraka, pamoja na kuendesha shughuli zao za biashara na kijamii kwa ufanisi.

“Huduma hizi zimefungua dunia kwa wananchi waliokuwa hawajawahi kupata mawasiliano kabisa,” alisema Ching’uli.

Aidha, Bw. Ching’uli ameongeza kuwa TTCL kama mtoa huduma wa ndani inaendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha huduma zinafika hadi maeneo ya pembezoni ambayo bado hayajafikiwa.

Amesema kuwa pamoja na changamoto za miundombinu na jiografia ya maeneo mengi ya Nkasi, shirika lao limejipanga kuhakikisha kuwa kila mnara unaojengwa unatoa huduma bora na za uhakika kwa wananchi.

Aliwataka wananchi kutumia miundombinu hiyo kwa tija ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika jamii zao.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongolo Nyerere ametumia wasaa huo kuishukuru serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote UCSAF kwa kupeleka huduma ya mawasiliano katika mkoa huo.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

TUME YATOA MAELEKEZO YA KISERA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025

October 23, 2025

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UCHAGUZI WA UDIWANI KATIKA KATA YA NYAKASUNGWA JIMBO LA BUCHOSA

October 18, 2025

RC Malisa Azindua Wodi ya Watoto Wachanga Hospitali ya Meta Mbeya kwa Ushirikiano wa IHI na NEST360 Tanzania

October 18, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025222

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025199

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024194

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025126
Don't Miss

Nilivyookoa Ndoa Yangu Baada ya Migogoro Kila Usiku Kuhusu Pesa na Wivu

By Mbeya YetuOctober 27, 20251

Ndoa yangu ilifika hatua ya kutisha. Kila usiku tulikuwa tukilumbana kuhusu kitu kipya, hasa pesa…

MWAKIPESILE: ”TUKAANDAMANE OKTOBA 29 KWA AJILI KUWAPIGIA KURA VIONGOZI KWA AMANI”

October 27, 2025

“Tunatiki CCM, Tunatunza Amani” — Kauli ya Bodaboda Kiwira Yakonga Moyo wa Suma Fyandomo

October 27, 2025

Nilivyomfanya Mtu Aliyenidharau Kuniheshimu na Kunitegemea Kwa Mambo Mengi

October 27, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Nilivyookoa Ndoa Yangu Baada ya Migogoro Kila Usiku Kuhusu Pesa na Wivu

October 27, 2025

MWAKIPESILE: ”TUKAANDAMANE OKTOBA 29 KWA AJILI KUWAPIGIA KURA VIONGOZI KWA AMANI”

October 27, 2025

“Tunatiki CCM, Tunatunza Amani” — Kauli ya Bodaboda Kiwira Yakonga Moyo wa Suma Fyandomo

October 27, 2025
Most Popular

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025222

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025199

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024194
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.