Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Kijana Asiyeamini Katika Bahati Anashangaza Wote Baada ya Kushinda Kiasi Kikubwa Kwenye Bet

October 25, 2025

Nilivyopata Flat Tummy Baada ya Kuteseka na Kitambi kwa Miaka Mitatu

October 24, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Beno Malisa Atoa Rai ya Kudumisha Amani Kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29

October 24, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Kijana Asiyeamini Katika Bahati Anashangaza Wote Baada ya Kushinda Kiasi Kikubwa Kwenye Bet
  • Nilivyopata Flat Tummy Baada ya Kuteseka na Kitambi kwa Miaka Mitatu
  • Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Beno Malisa Atoa Rai ya Kudumisha Amani Kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29
  • MKONGOMAN ATOA USHUHUDA MZITO KUTOWEKA KWA AMANI NCHINI JAMHURI YA KONGO
  • DKT HARRISON MWAKYEMBE ATOA SOMO ZITO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
  • DC ITUNDA ATETA NA WANA VICOBA AWAPA NENO HILI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKT 29
  • WANANCHI KATA IGANZO MTAA MWAMBENJA WAISHUKURU MBEYA UWSA KWA MRADI WA MAJITAKA
  • TUME YATOA MAELEKEZO YA KISERA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » WATENDAJI UCHAGUZI WATAKIWA KUFANYA VIKAO NA VYAMA VYA SIASA
Habari za Kitaifa

WATENDAJI UCHAGUZI WATAKIWA KUFANYA VIKAO NA VYAMA VYA SIASA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuJuly 23, 2025No Comments17 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025. Mafunzo hayo yamefanyika mkoani Shinyanga kuanzia Julai 21 hadi 23 mwaka huu.  (Picha na INEC).

 

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 23, 2025. Mafunzo hayo yamefanyika mkoani Shinyanga kuanzia Julai 21 hadi 23 mwaka huu.  (Picha na INEC).
Mwenyekiti wa Mafunzo Ndg. Faustine Lagwen, akizungumza jambo.

 

Washiriki wakifuatilia ufungaji wa mafunzo hayo. 

 

Washiriki kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu wakifuatilia ufungaji wa mafunzo hayo.

Na. Mwandishi wetu.
Tume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi imewaelekeza watendaji wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kufanya vikao na
viongozi wa vyama vya siasa kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha kuwa uteuzi wa wagombea unafanyika kwa mujibu wa sheria.


Maelekezo hayo yametolewa na
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs
Mwambegele wakati akifunga mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi mkoani Shinyanga
leo Julai 23, 2025.

“Mtatakiwa kuyatafsiri mafunzo haya kwenye usimamizi wenu
wa shughuli za kila siku za masuala ya uchaguzi kwa kuanza na vikao na vyama
vya siasa, utoaji wa fomu za uteuzi na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge
na kuhakikisha utoaji wa fomu za uteuzi na uteuzi wenyewe ngazi ya udiwani
ufanyike kwa mujibu wa sheria,”
amesema.

Amewaelekeza kuitisha na kuratibu kamati za upangaji wa ratiba za kampeni
na kuitisha kamati za maadili iwapo kuna changamoto zitajitokeza wakati wa kampeni.

Jaji Mwambegele
amewakumbusha watedaji hao kuhusu wajibu wao wa kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa
uchaguzi ngazi ya vituo na kuratibu na kusimamia vizuri na kwa weledi uchaguzi
ngazi ya vituo.

“Mafunzo mtakayowapa yatawawezesha kuratibu na kusimamia
uchaguzi ngazi ya kata vizuri na kwa weledi. Hivyo, jukumu lenu ni kutoa
mafunzo sahihi, kwa kuonesha kwa vitendo yote wanavyotakiwa kuyafanya
wasimamizi wasaidizi ngazi ya Kata,” amesema.

Akifunga mafunzo kama hayo Kisiwani Pemba, Zanzibar, Makamu
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani (Mstaafu)
Mbarouk Salim Mbarouk amewakumbusha watendaji hao wajibu wao wa k
ubandika mabango, orodha ya majina ya wapiga kura na
matangazo au taarifa zinazopaswa kuwafikia wapiga kura kwa kuwa ni takwa la
kisheria na kanuni zinazosimamia uchaguzi.

“Ni wajibu wenu kuhakikisha mabango, matangazo, orodha ya majina ya wapiga
kura na taarifa yoyote inayotakiwa kubandikwa kulingana na kalenda ya
utekelezaji wa majukumu ya uchaguzi inabandikwa ili kuepusha malalamiko ya ukiukwaji
wa masharti ya sheria na kanuni za uchaguzi,” amesema.

Amewasisitiza watendaji hao kutoa taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya
habari ili kuwajulisha wananchi na wadau mambo mbalimbali ya uchaguzi.

“Hakikisheni mnajiandaa kabla ya kukutana na vyombo vya habari. Pima
taarifa yako unayotaka kuitoa kabla hujaitoa ili kuepuka kuleta taharuki badala
ya utulivu katika eneo lako na Taifa kwa ujumla,” amesema.

Mafunzo hayo yamefanyika kwa
siku tatu kwenye mikoa mbalimbali nchini na yanawajumuisha waratibu wa
uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya
jimbo.

Tume iliyagawa mafunzo hayo
kwenye awamu mbili ambapo awamu hii ya pili ilihusisha mikoa ya Simiyu,
Shinyanga, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Mwanza, Mara, Dar es Salaam, Pwani,
Rukwa, Katavi, Manyara, Arusha, Songwe na Mbeya.

Awamu ya kwanza ilifanyika
tarehe 15 hadi 17 na ilihusisha watendaji kutoka mikoa ya Morogoro, Singida,
Dodoma, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Mjini Magharibi, Geita, Kagera,
Mtwara, Lindi, Tabora, Kigoma, Tanga, Kilimanjaro, Ruvuma, Iringa na Njombe.
Mwisho.
Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

TUME YATOA MAELEKEZO YA KISERA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025

October 23, 2025

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UCHAGUZI WA UDIWANI KATIKA KATA YA NYAKASUNGWA JIMBO LA BUCHOSA

October 18, 2025

RC Malisa Azindua Wodi ya Watoto Wachanga Hospitali ya Meta Mbeya kwa Ushirikiano wa IHI na NEST360 Tanzania

October 18, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025222

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025194

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024194

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025126
Don't Miss
Uncategorized

Kijana Asiyeamini Katika Bahati Anashangaza Wote Baada ya Kushinda Kiasi Kikubwa Kwenye Bet

By Mbeya YetuOctober 25, 20250

Kwa muda mrefu, Paul alikuwa mmoja wa wale vijana waliokuwa hawaamini kabisa katika bahati. Kila…

Nilivyopata Flat Tummy Baada ya Kuteseka na Kitambi kwa Miaka Mitatu

October 24, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Beno Malisa Atoa Rai ya Kudumisha Amani Kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29

October 24, 2025

MKONGOMAN ATOA USHUHUDA MZITO KUTOWEKA KWA AMANI NCHINI JAMHURI YA KONGO

October 23, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Kijana Asiyeamini Katika Bahati Anashangaza Wote Baada ya Kushinda Kiasi Kikubwa Kwenye Bet

October 25, 2025

Nilivyopata Flat Tummy Baada ya Kuteseka na Kitambi kwa Miaka Mitatu

October 24, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Beno Malisa Atoa Rai ya Kudumisha Amani Kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29

October 24, 2025
Most Popular

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025222

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025194

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024194
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.