Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

Nilikuwa naishi kwenye banda la mabati sasa majirani wanapiga picha kwenye nyumba yangu ya ghorofa

July 31, 2025

“MAHUNDI: Uongozi Wangu ni kwa Wanawake wa Mbeya – Asanteni kwa kuniamini tena

July 31, 2025

“SUMA FYANDOMO: Nitajifunza na Kushirikiana Nanyi! Aibuka na kura 1152.

July 31, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • Nilikuwa naishi kwenye banda la mabati sasa majirani wanapiga picha kwenye nyumba yangu ya ghorofa
  • “MAHUNDI: Uongozi Wangu ni kwa Wanawake wa Mbeya – Asanteni kwa kuniamini tena
  • “SUMA FYANDOMO: Nitajifunza na Kushirikiana Nanyi! Aibuka na kura 1152.
  • Nilivyoweza kurejesha heshima ndani ya ndoa yangu
  • KUMEKUCHA!! WATEULE SITA UBUNGE CCM JIMBO MBEYA MJINI WAANZA KUUZA SERA ZAO KWA WAJUMBE,KATIKA KATA
  • Niliwahi kuandikiwa wasifu wa kifo Hospitalini ila leo nawambia siri ya kupona
  • HUJUMA NYINGINE KUBWA WIZI DHIDI YA MAJI MAMLAKA YA MAJI MBEYA
  • Nilipigwa na butwaa kuona jina lake kwenye hati ya shamba la Sugar Daddy
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » WATANZANIA MILIONI 37 KUPIGA KURA TAREHE 29 OKTOBA, 2025
Habari za Kitaifa

WATANZANIA MILIONI 37 KUPIGA KURA TAREHE 29 OKTOBA, 2025

Mbeya YetuBy Mbeya YetuJuly 26, 2025Updated:July 26, 2025No Comments15 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa kalenda ya uchaguzi Mkuu 2025 katika hafla iliyofanyika Ofisi za Tume Njedengwa Jijini Dodoma Julai 26,2025. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa Tume, Ndg. Kailima Ramadhani.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kalenda ya uchaguzi Mkuu 2025 katika hafla iliyofanyika Ofisi za Tume Njedengwa Jijini Dodoma Julai 26,2025. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa Tume, Ndg. Kailima Ramadhani.

 

Sehemu ya viongozi kutoka vyama mbalimbali vya siasa vilivyohudhuria hafla ya uzinduzi wa uzinduzi rasmi wa kalenda ya uchaguzi Mkuu 2025 katika hafla iliyofanyika Ofisi za Tume Njedengwa Jijini Dodoma Julai 26,2025. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa Tume, Ndg. Kailima Ramadhani.

 

 

Sehemu ya viongozi kutoka vyama mbalimbali vya siasa vilivyohudhuria hafla ya uzinduzi wa uzinduzi rasmi wa kalenda ya uchaguzi Mkuu 2025 katika hafla iliyofanyika Ofisi za Tume Njedengwa Jijini Dodoma Julai 26,2025. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa Tume, Ndg. Kailima Ramadhani.

 

 

 

 

******

Na. Mwandishi Wetu
Tarehe 29 Oktoba, 2025 ndio siku ya
Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani
kwa Tanzania Bara. Jumla ya Wapiga Kura 37,655,559 wamejiandikisha.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume
Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele leo
tarehe 26 Julai, 2025 kwenye hafla ya uzinduzi wa ratiba ya uchaguzi
iliyofanyika kwenye makao makuu ya Tume, Njedengwa jijini Dodoma.

“Tarehe 09 Agosti, 2025 hadi tarehe 27
Agosti, 2025 itakuwa utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais na
Makamu wa Rais. Tarehe 14 Agosti, 2025 hadi tarehe 27 Agosti, 2025 itakuwa
utoaji wa fomu za uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani na tarehe 27 Agosti,
2025 itakuwa siku ya uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais,
uteuzi wa wagombea ubunge na uteuzi wa wagombea udiwani,” amesema Jaji
Mwambegele na kuongeza…..

“Tarehe 28 Agosti, 2025 hadi tarehe 28
Oktoba, 2025 kitakuwa kipindi cha kampeni za uchaguzi kwa Tanzania Bara. Tarehe
28 Agosti, 2025 hadi 27 Oktoba, 2025 kitakuwa kipindi cha kampeni za Uchaguzi
kwa Tanzania Zanzibar ili kupisha kura ya mapema na Tarehe 29 Oktoba, 2025 siku
ya Jumatano itakuwa ndiyo Siku ya Kupiga Kura”.

Akazingumza kuhusu idadi ya wapiga kura
waliojiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi huo, Jaji Mwambegele amesema jumla
ya wapiga kura 37,655,559 wamejiandikisha na kuongeza kuwa idadi hiyo ni sawa
na ongezeko la asilimia 26.55 kutoka idadi ya wapiga kura 29,754,699 waliokuwa
kwenye daftari, mwaka 2020.

Ameongeza kuwa kwa upande wa Zanzibar,
Wapiga Kura 725,876 wapo katika Daftari la Wapiga Kura la Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar (ZEC) na wapiga kura 278,751 wameandikishwa na INEC kwa kuwa hawakuwa
na sifa za kuandikishwa na ZEC.

“Katika idadi ya wapiga kura 37,655,559
waliopo katika daftari, wapiga kura 36,650,932 wapo Tanzania Bara na wapiga kura
1,004,627 wapo Tanzania Zanzibar,” amesema Jaji Mwambegele.

Ameongeza kuwa kati ya wapiga kura hao,
18,943,455 ni wanawake sawa na asilimia 50.31 na wapiga kura 18,712,104 ni
wanaume sawa na asilimia 49.69 na wapiga kura 49,174 ni watu wenye ulemavu.

Amesema jumla ya vituo 99,911
vitatumika kupigia kura ambapo vituo 97,349 vitatumika kwa ajili ya kupigia
kura kwa Tanzania Bara na vituo 2,562 vitatumika kwa ajili ya kupigia kura kwa
Tanzania Zanzibar.

“Idadi hii ya vituo 99,911 ni sawa na
ongezeko la asilimia 22.49 ya vituo vya kupigia kura 81,567 vilivyotumika
katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020,” amesema.

Jaji Mwambegele ametoa wito kwa wadau
wote ikiwa ni pamoja na wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa
uchaguzi kwa kuzingatia sheria, kanuni, miongozo na maelekezo yatakayotolewa na
Tume.

 

 

 

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

VYAMA VYA SIASA VYAHAKIKISHIWA UWANJA SAWA UCHAGUZI MKUU 2025

July 27, 2025

Daraja la Masagi Wilayani Iramba kufungua mawasiliano vijijini

July 24, 2025

Waziri Aweso Aagiza Mabomba Yote ya Mto Kiwira Yatengenezwe Mara Moja

July 24, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024177

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202485

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202580

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 202576
Don't Miss
Uncategorized

Nilikuwa naishi kwenye banda la mabati sasa majirani wanapiga picha kwenye nyumba yangu ya ghorofa

By Mbeya YetuJuly 31, 20250

Wakati wengine walikuwa wanazungumzia ndoto zao za kuishi kwenye majumba ya kifahari, mimi nilikuwa nalala…

“MAHUNDI: Uongozi Wangu ni kwa Wanawake wa Mbeya – Asanteni kwa kuniamini tena

July 31, 2025

“SUMA FYANDOMO: Nitajifunza na Kushirikiana Nanyi! Aibuka na kura 1152.

July 31, 2025

Nilivyoweza kurejesha heshima ndani ya ndoa yangu

July 30, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

Nilikuwa naishi kwenye banda la mabati sasa majirani wanapiga picha kwenye nyumba yangu ya ghorofa

July 31, 2025

“MAHUNDI: Uongozi Wangu ni kwa Wanawake wa Mbeya – Asanteni kwa kuniamini tena

July 31, 2025

“SUMA FYANDOMO: Nitajifunza na Kushirikiana Nanyi! Aibuka na kura 1152.

July 31, 2025
Most Popular

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024177

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202485

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202580
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.