Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

USHIRIKI BENKI NMB MAONESHO KILIMO NANE NANE MBEYA,ELIMU UJASIRIAMALI HUDUMA ZA KIBENKI ZATOLEWA

August 5, 2025

“Rais wa IPU Dkt. Tulia Kuongoza Uzinduzi wa Kitabu cha Ndoto ya Yatima”Mbeya, Septemba 13

August 5, 2025

Aliyenitapeli mtandaoni anirudishia fedha zangu

August 5, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • USHIRIKI BENKI NMB MAONESHO KILIMO NANE NANE MBEYA,ELIMU UJASIRIAMALI HUDUMA ZA KIBENKI ZATOLEWA
  • “Rais wa IPU Dkt. Tulia Kuongoza Uzinduzi wa Kitabu cha Ndoto ya Yatima”Mbeya, Septemba 13
  • Aliyenitapeli mtandaoni anirudishia fedha zangu
  • Mwamba atangaza ndoa na Bibi wa miaka 84, ataja sababu
  • TCRA Yapaza Sauti Kupitia Kisaka: Bloga Muwe Mabalozi wa Amani Uchaguzi 2025
  • WATOTO WA VIJIJI VYA USANGU MBARALI MBEYA WASHINDANA KUSOMA VITABU WAJENGEWA HAMASA YA KUSOMA
  • Mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi Ngazi ya kata jimbo la Mbeya Yasisitiza Utii wa Sheria
  • TANZANIA WENYEJI WA WARSHA YA WAKUU WA TAASISI ZA KUPAMBANA NA RUSHWA KUTOKA NCHI ZA SADC
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home ยป TANZANIA WENYEJI WA WARSHA YA WAKUU WA TAASISI ZA KUPAMBANA NA RUSHWA KUTOKA NCHI ZA SADC
Habari za Kitaifa

TANZANIA WENYEJI WA WARSHA YA WAKUU WA TAASISI ZA KUPAMBANA NA RUSHWA KUTOKA NCHI ZA SADC

Mbeya YetuBy Mbeya YetuAugust 4, 2025No Comments18 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Arusha, Agosti 4, 2025

Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa Warsha ya Wakuu wa Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), itakayofanyika kwa siku tatu kuanzia Agosti 4 hadi 6, 2025, katika Hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha.

Warsha hii ya kimataifa inafanyika wakati Tanzania ikiwa na jukumu la Uenyekiti wa Kamati ya Kupambana na Rushwa ya SADC (SADC Anti-Corruption Committee – SACC) kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), nafasi ambayo ilianza rasmi Oktoba 2, 2024.

Hii ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya nchi wanachama chini ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC ambayo kwa sasa inaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tangu Agosti 17, 2024.

Warsha hiyo pia itaambatana na maadhimisho ya miaka 20 ya utekelezaji wa Itifaki ya SADC Dhidi ya Rushwa, itifaki ambayo ilianza kutekelezwa rasmi Julai 2005 kwa lengo la kuimarisha mifumo ya kuzuia, kugundua, kuadhibu na kutokomeza rushwa katika sekta za umma na binafsi ndani ya nchi wanachama.

Malengo mahsusi ya warsha hii ni pamoja na:

  1. Kutafakari miaka 20 ya utekelezaji wa Itifaki ya SADC Dhidi ya Rushwa โ€“ mafanikio na changamoto.

  2. Kutathmini mafanikio yaliyopatikana na kubaini mapungufu katika sheria, uwezo wa taasisi na ushirikiano wa kikanda.

  3. Kuweka vipaumbele vya kimkakati kwa mustakabali wa mapambano dhidi ya rushwa katika ukanda wa SADC.

Katika warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Francis Chalamila, ambaye pia ni Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa SACC, atakabidhi rasmi kijiti cha Uenyekiti kwa mwakilishi kutoka nchi ya Malawi.

Ni muhimu kukumbusha kwamba Tanzania ilipongezwa na Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa SADC katika mkutano wao wa 27 uliofanyika Julai 21โ€“25, 2025 jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo, Katibu Mtendaji wa SADC, Elias Magosi, alisifu juhudi za Tanzania katika mapambano dhidi ya rushwa, akieleza kuwa nchi imeonesha mafanikio makubwa katika maeneo ya mifumo ya kisheria, dhamira ya kisiasa na ushiriki wa wadau.

Kupata heshima ya kuwa mwenyeji wa warsha hii ni ushahidi wa nafasi ya Tanzania katika juhudi za kimataifa za kupambana na rushwa, kuimarisha utawala bora, kuendeleza amani na kukuza maendeleo ya kiuchumi katika kanda.

TAKUKURU imesisitiza kuwa imejipanga kuhakikisha kuwa maazimio ya warsha hii yatakuwa na mchango chanya kwa taifa na ukanda wa SADC kwa ujumla.


Mwisho
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano โ€“ TAKUKURU
Arusha, Tanzania

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

TCRA Yapaza Sauti Kupitia Kisaka: Bloga Muwe Mabalozi wa Amani Uchaguzi 2025

August 4, 2025

WAZALISHAJI WA MAUDHUI MTANDAONI WAHIMIZWA KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025

August 4, 2025

WAANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUHAMASISHA USHIRIKI WA WANANCHI KUPIGA KURA

August 2, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024179

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025157

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202485

UCHAGUZI MKUU 2025: MAJIMBO MAPYA NANE YAANZISHWA, 12 YABADILISHWA MAJINA

May 12, 202581
Don't Miss
Video Mpya

USHIRIKI BENKI NMB MAONESHO KILIMO NANE NANE MBEYA,ELIMU UJASIRIAMALI HUDUMA ZA KIBENKI ZATOLEWA

By Mbeya YetuAugust 5, 20250

#mbeyayetutv

“Rais wa IPU Dkt. Tulia Kuongoza Uzinduzi wa Kitabu cha Ndoto ya Yatima”Mbeya, Septemba 13

August 5, 2025

Aliyenitapeli mtandaoni anirudishia fedha zangu

August 5, 2025

Mwamba atangaza ndoa na Bibi wa miaka 84, ataja sababu

August 5, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

USHIRIKI BENKI NMB MAONESHO KILIMO NANE NANE MBEYA,ELIMU UJASIRIAMALI HUDUMA ZA KIBENKI ZATOLEWA

August 5, 2025

“Rais wa IPU Dkt. Tulia Kuongoza Uzinduzi wa Kitabu cha Ndoto ya Yatima”Mbeya, Septemba 13

August 5, 2025

Aliyenitapeli mtandaoni anirudishia fedha zangu

August 5, 2025
Most Popular

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024179

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025157

TULIA TRUST YATOA MIFUKO 400 YA SARUJI KWA SHULE 3 JIJINI MBEYA

March 26, 202485
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.