Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) Dkt. Tulia Ackson, ameendelea na Kampeni Zake za Kuomba ridhaa kwa Wananchi wa Jimbo hilo kumchagua kwa kura nyingi kwa nafasi yake ya Ubunge na kura nyingi kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya Urais katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 ili wakaendelee kutatua Changamoto zinazowakabili ikiwemo upatikanaji wa Soko la Kisasa ndani ya Mtaa wa Ituha Kata ya Ilomba.
Akizungumza mbele ya Wananchi wa kata ya Ilomba Katika Mitaa wa Ituha leo tarehe 23 Septemba, 2025 , Dkt. Tulia amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kimejipanga Kufanya kazi Kama ambavyo Kimefanya awamu zilizopita Katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Nishati na Miundombinu hivyo Wananchi Wanapaswa Kuwa na imani kubwa.
Katika hatua nyingine, Dkt. Tulia amesema katika sekta ya Elimu ndani ya kata ya Ilomba CCM imejenga Shule ya Msingi Tonya, imejenga Madarasa Mapya na Kuboresha Mazingira ya Elimu Sambamba na Kumaliza tatizo la uhaba wa Madawati, imeboresha Miundombinu ya Shule ya Sekondari Ilomba na Kujenga Shule ya Sekondari Ikulu sambamba na kutoa Vifaa vya Shule (Daftari) na Sare za Shule kwa wanafunzi wanaotoka Kwenye Mazingira Magumu ili watoto wa Ilomba wapate elimu bora na hayo yote yataendelea kufanyika endapo wataipa dhamana CCM.
Hali kadhalika, Dkt. Tuliaameongeza kuwa, aanatarajia kuboreha Miundombinu Katika sekta ya Elimu ikiwemo Ukarabati wa Madarasa Kwa Shule zote za Msingi na Sekondari, Kumaliza Changamoto ya Maji Kupitia Mradi wa Mto Simba utakaopeleka Maji ndani ya Kata hiyo kwani tayari utekekelezaji wake umeanza na pia Mradi Mkubwa wa Mto Kiwira utamaliza Kabisa tatizo la Maji, Kuhakikisha zahanati ya Ilomba inatoa huduma zilizo bora na pia Kujenga Kituo cha Afya na Kuboresha zaidi huduma Katika Hospitali ya Wilaya ya Igawilo ikiwemo Kuongeza Wahudumu na Kutoa Bima za Afya Kwa wote hususani Kaya zisizojiweza.
Katika hatua Nyingine, Dkt .Tulia amesema atahakikisha Barabara ndani ya Kata ya Ilomba zinajengwa Kwa Kiwango Cha lami pamoja na kuunganisha Kata ya Ilomba na Uyole kupitia Barabara ya Roma Ituha Kwenda Nsongwi Juu na kuzifanya Barabara za Mitaa zipitike nyakati zote.
Kampeni za jimbo la Uyole zinapambwa na kaulimbiu ya “Uyole Kazi” ikilenga Kufanya kazi Kwa Maarifa na Nguvu Zaidi.