Leo 29 Oktoba 2025 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole kwa tiketi ya CCM Dkt Tulia Ackson ameendela na Kampeni zake za kuinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Kata ya Ilemi ambapo amewahidi Wakazi wa eneo hilo Kuhakikisha Barabara ya Juhudi ambayo ni kero Kubwa kwa Wananchi inajengwa kwa Kiwango cha Lami kama ya Mapelele.
Dkt. Tulia amesema wakati anaomba ridhaa ya kuliongoza Jimbo la Mbeya Mjini aliahidi Kujenga Barabara ya Mapelele ambayo tayari imekamilika, Pia aliahidi Ujenzi wa Barabara njia Nne ambayo Ujenzi wake unaendelea hivyo kwa sasa atahakikisha Barabara ya Juhudi na Ile ya kwenda Kituo cha Afya zinajengwa.
Akizungumza Mbele ya Wananchi wa Ilemi Kwenye Mkutano wake wa Kampeni eneo la Uwanja wa James amesema Sambamba na Barabara hizo pia atahakikisha Barabara ya Kuunganisha Ilemi na Kata ya Mwansenkwa inajengwa, Mitaro Mikubwa na Vivuko vyote vitajengwa ili kurahisisha Shughuri za Usafiri na kuwaunganisha Wakazi wa Jimbo la Uyole kwa Barabara za Lami.
Sambamba na hayo Dkt. Tulia ameeleza Mambo atakayoyafanya ndani ya Jimbo la Uyole na Kata hiyo ikiwa ni Pamoja na Kujenga na Kukarabati Madarasa ya Shule zote kata ya Ilemi, kuboresha huduma za Afya ndani ya Kituo cha Afya Ilemi na Hospitali ya Igawilo, Kuwainua Wananchi wa Uyole Kiuchumi na Kutatua Changamoto ya upatikanaji wa Maji.
Mkutano huo wa Kampeni za Dkt Tulia umehudhuriwa na Naibu katibu Mkuu wa Jumuia ya Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndg. Kilumbe Ng’enda ambaye amewapongeza Wananchi wa Jimbo la Uyole kwa Kumpa ridhaa Dkt. Tulia Ackson kuwa Mbunge awamu iliyopita kwani Kiongozi huyo amefanya Kazi nzuri katika nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania na Umoja wa Mbunge Dunia (IPU) na amewataka wajitokeze kupiga Kura nyingi kwa Wagombea wa CCM 29 Oktoba 2025 ili Waendelee kuwaletea Maendeleo.
Kampeni za Jimbo la Uyole zinapambwa na kaulimbiu ya “Uyole Kazi” ikilenga Kufanya kazi Kwa Maarifa na Nguvu Zaidi.