Kampeni za Uchaguzi Mkuu zinaendelea kwa kasi katika Jimbo la Mbarali, ambapo Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Bahati Keneth Ndingo, ameendelea na ziara yake ya kuomba kura kwa wananchi na wanachama wa CCM katika Kata ya Rujewa na maeneo ya jirani yanayo unda kata hiyo
Katika ziara hiyo ya leo, Mhe. Bahati Ndingo ametembelea maeneo mbalimbali ya Kata ya Rujewa, yakiwemo maeneo ya: Ihanga, Luwilindi, Mkwajuni, Rujewa Mjini, Mabanda, na Ibara, ambapo amekuwa akizungumza moja kwa moja na wananchi, akiwasihi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, na kuwachagua wagombea wote wa CCM kuanzia nafasi ya Urais, Ubunge hadi Udiwani.
Aidha Bahati Ndingo Amemshukuru Mgombea wanafasi ya Urais wa chama cha mapinduzi CCM DKT, Samia suluhu Hassani Kwa kazi kubwa alizozifanya katika Jimbo la Mbarali Kwa kuleta fedha nyingi za miradi kwaajili ya wananchi wa Mbarali , hivyo amewasihi wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi CCM kumuunga mkono Kwa kupiga kura nyingi za Ndiyo kama ishara ya kurudisha shukrami kazi kubwa alizozifanya Mbarali
Katika ziara hiyo Mgombea Ubunge Bahati Ndingo amefanya mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Starlight, Rujewa, ambapo ameinadi Ilani ya CCM ya mwaka 2025 – 2030, huku akielezea mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kupitia chama hicho ndani ya kata hiyo, Pia ameeleza kuwa serikali ya CCM imeweza kutekeleza miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 2.5, ikiwa ni pamoja na miradi ya elimu, afya, miundombinu, na miradi ya maji
Ziara hiyo imeendelea kuimarisha uungwaji mkono kwa CCM katika Jimbo la Mbarali, huku wananchi wengi wakionesha matumaini makubwa kwa utekelezaji wa ahadi za chama hicho endapo kitapewa ridhaa ya kuendelea kushika Dora
Kampeni hizi zinaongozwa na kaulimbiu ya “Tunaendeleza Tulipoishia – Mbarali Yetu, Fahari Yetu” Kauli mbiu hii ikiwa inalenga na kusisitiza Kazi, Maarifa, Nguvu, na kujituma zaidi kwa maendeleo ya wananchi.
📲 Endelea kufuatilia taarifa na matukio ya kampeni ya Mhe. Bahati Keneth Ndingo kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii.
🔰 @Bahati Keneth Ndingo
#BKN #CCM2025 #MbaraliKwanza