Close Menu
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.

What's Hot

WILAYA YA RUNGWE YAMKABIDHI RASMI MKANDARASI WA KAGWA GENERAL SUPPLIES KUANZA KUJENGA SOKO LA NDIZI LA KISASA KIWILA

November 26, 2025

*DKT. MWIGULU AWAONYA WAVUNJIFU WA SHERIA*

November 26, 2025

WILAYA YA RUNGWE YAMKABIDHI RASMI MKANDARASI WA KAGWA GENERAL SUPPLIES KUANZA KUJENGA SOKO LA NDIZI

November 26, 2025
Facebook X (Twitter) Instagram
Trending
  • WILAYA YA RUNGWE YAMKABIDHI RASMI MKANDARASI WA KAGWA GENERAL SUPPLIES KUANZA KUJENGA SOKO LA NDIZI LA KISASA KIWILA
  • *DKT. MWIGULU AWAONYA WAVUNJIFU WA SHERIA*
  • WILAYA YA RUNGWE YAMKABIDHI RASMI MKANDARASI WA KAGWA GENERAL SUPPLIES KUANZA KUJENGA SOKO LA NDIZI
  • Karejesha tabasamu la uso wake na ndoa yake
  • HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YAANZA RASMI KUTOA MAFUNZO YA HUDUMA ZA DHARURA KWA LENGO LA KUOKOA MAISHA NA KUPUNGUZA ATHARI ZA AJALI NA DHARURA ZA KIAFYA NYANDA ZA JUU KUSINI
  • TANZANIA NA QATAR ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA KUTAMBULIANA VYETI VYA MABAHARIA
  • EDEN KATININDA: ”MNUNUZI MASHUHURI WA PARETO NCHINI ATOA SOMO KWA WAKULIMA WA ZAO LA PARETO”
  • Anapokea mshahara mzuri na mazingira rafiki ya kazi
Facebook X (Twitter) Instagram
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
  • Home
  • Habari za Kitaifa
  • Utalii na Utamaduni
  • Elimu na Vijana
  • Matukio ya Kijamii
  • Afya na Ustawi
Mbeya Yetu OnlineMbeya Yetu Online
Home » WILAYA YA RUNGWE YAMKABIDHI RASMI MKANDARASI WA KAGWA GENERAL SUPPLIES KUANZA KUJENGA SOKO LA NDIZI LA KISASA KIWILA
Habari za Kitaifa

WILAYA YA RUNGWE YAMKABIDHI RASMI MKANDARASI WA KAGWA GENERAL SUPPLIES KUANZA KUJENGA SOKO LA NDIZI LA KISASA KIWILA

Mbeya YetuBy Mbeya YetuNovember 26, 2025Updated:November 26, 2025No Comments5 Views
Facebook Twitter Pinterest LinkedIn WhatsApp Reddit Tumblr Email
Share
Facebook Twitter LinkedIn Pinterest Email

Rungwe, Tanzania – Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imekamilisha hatua ya awali ya mradi mkubwa wa Soko la Kisasa la Ndizi lenye thamani ya Shilingi bilioni 2.8, hatua inayofungua ukurasa mpya wa maendeleo kwa wakulima na wafanyabiashara wa eneo hilo na mikoa ya jirani.

Akizungumza wakati wa hafla ya leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Bwana Renatus Mchau, amesema hatua hii ni kumkabidhi mkandarasi site pamoja na kuhakikisha taratibu zote za kimkataba zimekamilika.

“Leo hii tumekamilisha taratibu zote za kimkataba. Zoezi la leo ni kumkabidhi mkandarasi site, kuhakikisha kila kitu kipo sawa kabla ya kuanza ujenzi rasmi,” alisema Mchau.

Mkurugenzi Mtendaji aliishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wizara ya Tamisemi, Wizara ya Fedha, na Wizara ya Kilimo kwa mchango wao wa kitaalam katika hatua zote za maandalizi ya mradi. Alihakikisha kuwa wananchi, wafanyabiashara na wakulima ambao kwa muda mrefu wamepitia changamoto mbalimbali katika eneo hilo, wanapaswa kuwa wanufaika wakubwa wa mradi huu.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Kagwa General Supplies Limited, Bwana Emmanuel Madaffa, amesema serikali imeonyesha imani kubwa kwa kutoa fursa kwa wazawa kutekeleza mradi huo badala ya wageni.

“Naiishukuru sana Serikali chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuamini sisi wazawa. Tunawaahidi kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha tunatimiza lengo la Serikali na kuondoa changamoto za muda mrefu kwa wananchi,” alisema Madaffa.

Amesema mradi huo utakuwa kichocheo muhimu cha maendeleo na utawanufaisha si tu wakulima wa Rungwe na Kyela, bali pia mikoa ya jirani. Kampuni tayari imekabidhiwa cheti cha kuanza kazi, hivyo shughuli zinaanza mara moja. Aidha, amewaasa wakandarasi kushirikiana na wahandisi na taasisi za kitaalamu, kuepuka ubadhirifu, na kutoa nafasi kwa vijana wa Rungwe kushiriki katika kazi ndogo zisizohitaji ujuzi.

Mbunge wa Jimbo la Rungwe, Mh. Mantona, amesema soko hilo ni mojawapo ya miradi mikubwa inayolenga kuboresha uchumi wa wakulima na wafanyabiashara wa eneo hilo, akibainisha kuwa litafungua fursa nyingi za kipato na kuongeza thamani ya mazao.

“Huu ni mradi mkubwa sana kwa watu wa Rungwe. Tukiuendeleza vizuri, manufaa yake yataonekana kwa wote—wakulima, wafanyabiashara, na jamii kwa ujumla,” alisema Mbunge Mantona.

Soko hili la kisasa linatarajiwa kuwa suluhu ya kudumu kwa changamoto ya masoko kwa wakulima wa ndizi, litakaloongeza thamani ya zao hilo, na kuvutia wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi.

Mwisho, Afisa Tawala Amimu Mwandelile, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya Rungwe, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano, uwazi na kufuata taratibu zote za kiserikali katika utekelezaji wa mradi.

“Njia bora ya kutatua changamoto ni kupitia vikao na majadiliano ya pamoja. Viongozi, wafanyabiashara na wahandisi wanapaswa kushirikiana ili mradi uendelee bila matatizo,” alisema Mwandelile.

Amewaasa wakandarasi kushirikiana na taasisi za kitaalamu, kuzingatia mkataba, na kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa viwango vinavyotarajiwa. Pia alisisitiza kuepuka haraka isiyo na mpangilio, ubadhirifu au ubinafsi, akibainisha kuwa kila hatua inapaswa kufuata mpangilio thabiti ili kufanikisha mradi.

“Tukiongoza mradi huu vizuri na kushirikiana kwa uwazi, tutapata matokeo bora. Mradi ni mali ya wananchi na kila mmoja ana wajibu wa kulinda ubora wake,” aliongeza.

Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Telegram Email
Mbeya Yetu

Related Posts

TANZANIA NA QATAR ZASAINI HATI YA MAKUBALIANO YA KUTAMBULIANA VYETI VYA MABAHARIA

November 26, 2025

DKT. MWIGULU: TANZANIA NI MALI YETU SOTE, SI MALI YA SERIKALI WALA CHAMA CHA SIASA

November 25, 2025

WAZIRI NANAUKA ATAKA VIJANA WASIKILIZWE

November 25, 2025

Leave A Reply Cancel Reply

Top Posts

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025236

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025230

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024201

WAHITIMU WA UUGUZI NA UKUNGA WAPEWA WITO WA KUONYESHA MAADILI, UPENDO NA HESHIMA KAZINI

August 28, 2025128
Don't Miss
Habari za Kitaifa

WILAYA YA RUNGWE YAMKABIDHI RASMI MKANDARASI WA KAGWA GENERAL SUPPLIES KUANZA KUJENGA SOKO LA NDIZI LA KISASA KIWILA

By Mbeya YetuNovember 26, 20255

Rungwe, Tanzania – Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imekamilisha hatua ya awali ya mradi mkubwa…

*DKT. MWIGULU AWAONYA WAVUNJIFU WA SHERIA*

November 26, 2025

WILAYA YA RUNGWE YAMKABIDHI RASMI MKANDARASI WA KAGWA GENERAL SUPPLIES KUANZA KUJENGA SOKO LA NDIZI

November 26, 2025

Karejesha tabasamu la uso wake na ndoa yake

November 26, 2025
Stay In Touch
  • Facebook
  • Twitter
  • Pinterest
  • Instagram
  • YouTube
  • Vimeo

Subscribe to Updates

Get the latest creative news from SmartMag about art & design.

About Us
About Us

Mbeya Yetu is a dynamic online platform that serves as a comprehensive source for news and information, offering a diverse range of content that caters to the interests and needs of its audience. Focusing on key pillars such as Habari za Kijamii (Social News), Uchumi na Biashara (Economy and Business), Elimu na Vijana (Education and Youth), Afya na Ustawi (Health and Well-being), and Habari za Kitaifa (National News), Mbeya Yetu is committed to keeping its community informed and engaged.

Facebook X (Twitter) Pinterest YouTube WhatsApp
Our Picks

WILAYA YA RUNGWE YAMKABIDHI RASMI MKANDARASI WA KAGWA GENERAL SUPPLIES KUANZA KUJENGA SOKO LA NDIZI LA KISASA KIWILA

November 26, 2025

*DKT. MWIGULU AWAONYA WAVUNJIFU WA SHERIA*

November 26, 2025

WILAYA YA RUNGWE YAMKABIDHI RASMI MKANDARASI WA KAGWA GENERAL SUPPLIES KUANZA KUJENGA SOKO LA NDIZI

November 26, 2025
Most Popular

Njia rahisi ya kushinda kesi Mahakamani bila kutoa rushwa

February 7, 2025236

LIVE: CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE BAADA YA KIKAO CHA KAMATI KUU (CCM)

July 29, 2025230

KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

March 19, 2024201
© 2025 Mbeya Yetu. Powered by Digital Media Innovation Program.
  • Home

Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.