Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Mhe. Bahati Kenneth Ndingo, amekabidhi mashuka kwa Kituo cha Afya Utengule ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Maadhimisho hayo yamefanyika katika Kata ya Utengule Usongwe, wilayani Mbarali.
Hatua hiyo inalenga kuboresha mazingira na huduma kwa wagonjwa wanaofika kupata matibabu katika kituo hicho cha afya. Baadhi ya wananchi wameeleza kuwa msaada huo utasaidia kupunguza changamoto zilizokuwepo awali na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya.

