Meneja Uhamasishaji Uwekezaji kutoka TISEZA, Daudi Riganda, amesema mamlaka hiyo inaendelea kuhamasisha uwekezaji ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza fursa za biashara nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea mradi wa Babito Trading Company katika Mbeya, alisema uwekezaji huo unaomilikiwa kwa asilimia 100 na Watanzania umegharimu zaidi ya shilingi bilioni nane.
Alisema mradi huo ni chanzo cha mapato kwa jiji la Mbeya na pia kwa TRA, huku ukiwa mfano wa mafanikio ya uwekezaji wa ndani kutokana na mazingira mazuri ya biashara yaliyopo Tanzania.
Aidha, alibainisha kuwa motisha za uwekezaji, ikiwemo punguzo la kodi na unafuu wa ushuru kwa baadhi ya vifaa vilivyoagizwa kutoka China, zimechangia kupunguza gharama za mradi.

