Mtu anayedaiwa kuwa mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya, Tido Kadaga (20), amekutwa amefariki dunia baada ya mwili wake kuonekana ukielea kwenye dimbwi la maji katika Mtaa wa Maili Tano, Kata ya Iganzo, Jijini Mbeya.
Kwa mujibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, walipokea taarifa kutoka kwa mashuhuda kuhusu mwili unaoelea majini na kufika eneo la tukio, kisha kuuopoa na kuupeleka Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya kwa uchunguzi zaidi.
Mrakibu Mwandamizi wa Zimamoto Mkoa wa Mbeya, Malumbo Ngata, amesema tukio hilo liliripotiwa majira ya mchana na baada ya uchunguzi wa awali kubainika marehemu ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza CBE.
Kwa upande wake, Mkuu wa chuo hicho, Dk Beny Mwenda, amesema wanangoja taarifa rasmi kutoka Jeshi la Polisi Tanzania kabla ya kutoa ufafanuzi zaidi.
Trending
- ZIMAMOTO WAOPOA MWILI WA KIJANA ALIYEDAIWA KUWA MWANAFUNZI WA CBE MBEYA
- Mvua na upepo mkali waathiri zaidi ya kaya 200 Mbeya
- TISEZA YASIFIA UWEKEZAJI WA BILIONI 8 WA BABITO TRADING COMPANY MBEYA
- AB YAPENDEKEZA MAPITIO MAKUBWA KULINDA BLOGA NA WATENGENEZA MAUDHUI
- SHEIKH WA MKOA MBEYA ATOA UJUMBE KWA WAISLAMU KUELEKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN
- EFTA YACHOCHEA UCHUMI KWA HATI FUNGANI YA BILIONI 50
- Kanisa la Moravian Tanzania Lamkabidhi Yona Sonelo Tuzo Maalum Baada ya Shahada ya Heshima Australia
- Beno Malisa Azindua Tawi la Strategies Insurance Mbeya, Akaribisha Wawekezaji

