Author: Mbeya Yetu

Mfanyabiashara maarufu wa Jijini Mbeya Josephat Mushi pamoja na dereva wa Gari lililobeba shehena ya samaki wenye thamani ya shilingi milioni 200 wamehukumiwa kwenda jela miaka 15 wakituhumiwa kwa makosa ya kukwepa ushuru,

Shehena hiyo ya samaki tani 26 zimeteketezwa katika Dampo la Jiji la Mbeya huku magari matatu yakiwemo Lori lililobeba shehena hiyo na magari mawili ya mfanyabiashara huyo yametaifishwa na serikali.

Read More

Taasisi ya Tanzania Yangu Entertainment imekuja na kitu kipya katika jamii ya walimbwende cha Miss Uzalendo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Yangu Ndele Mwanselela amesema kuwa lengo la kuanzisha Mashindano hayo ni kuwapandikiza Uzalendo wa nchi yao Walimbwende ikiwa ni pamoja na kuwaongezea weledi na Uelewa wa Mambo mbalimbali ya nchi yetu.

Read More

Mfumo mpya wa usimamizi wa fedha za Umma Epicor 10.2 umezinduliwa ukifuatiwa na mafunzo ya wiki tatu kwa watumishi 950 kutoka katika kada za Uhasibu na Mamlaka za Serikali za Mitaa 185 za Tanzania Bara(TAMISEMI).

Mafunzo haya yanaendeshwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani kupitia Mradi wa Maendeleo wa Kimataifa USAID.

Read More