Author: Mbeya Yetu

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amejipambanua kama mlezi wa Sekta binafsi nchini na hataki kuona wafanyabiashara wanapata misukosuko wakati wa utekelezaji wa majukumu Amesema maono ya Rais ni kujenga sekta binafsi itakayokuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye pato la Taifa na ili kufikia azma hiyo, viongozi wengine wahakikishe nia njema ya Rais kwa Wafanyabiashara inatekelezwa kwa vitendo.Amesema maono ya Rais ni kujenga sekta binafsi itakayokuwa na mchango mkubwa zaidi kwenye pato la Taifa na ili kufikia azma hiyo, viongozi wengine wahakikishe nia njema ya Rais kwa Wafanyabiashara…

Read More

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amewataka viongozi wa madhehebu ya kidini Nchini kuendekeza maridhiano ya amani ili kutunza amani na mshikamano uliopo katika Taifa.

Amezungumza hayo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Maridhiano Jijini Mbeya alipomwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye ukumbi wa Hotel ya Tughimbe.

Read More

Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo limesema litaendelea kutoa elimu kwa wafugaji na wafanya biashara wa Mifugo hapa Nchini huku likibainisha kuwa halitomwonea muhali mfugaji yeyote atakaye bainika kutorosha mifugo na kukiuka taratibu za uuzaji wa mifugo hapa nchini. Hayo yamebainisha leo Machi 09, 2024 Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora na Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo hapa nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua alipotembelea mnada wa Upili Igunga ambapo amebainisha kuwa kikosi hicho kitaendelea kutoa elimu kwa wafugaji Nchi nzima ili kuondokana uvunjifu wa sheria.  Wauza mifugo wa Mnada…

Read More

Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi- Arusha
Ikiwa leo ni Machi 08,2024 kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani, Mtaandao wa
Polisi Wanawake Mkoa wa Arusha wameunga na wanawake wengine Mkoani humo huku
Mtandao huo wakiitumia siku hiyo kuwawekea akiba ya fedha katika mfuko wa uwekezaji (UTT)
kwa Watoto wawili wa askari wanandoa waliofariki kwa ajali ya gari.
Akiongea katika Viwanja vya Ngarenaro Complex Jijini Arusha Mwenyekiti wa Mtandao huo
Mkoa wa Arusha Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema mtaandao huo
katika kuelekea kilele hicho ulianza mapema kutoa elimu maeneo mbalimbali Pamoja na
kufanya ibada ya kuwaombea marehemu.
SSP Zauda ameongeza kuwa katika kuadhimisha siku hiyo waliona vyema kuunga na
kuwawekea akiba ya fedha kwa Watoto wa askari wanandoa waliofariki katika ajali ya gari
ambapo amebainisha kuwa fedha hizo zitawasaidia Watoto hao katika swala la elimu na
mahitaji mengine ya kibinadamu.
Aidha ametoa wito kwa wanawake wengine Mkoani humo kufanya kazi kwa bidii,nidhamu na
kutenda haki ili ustawi bora na wajikwamue kiuchumi na maendeleo ya Taifa kwa Ujumla.
Nae mrakibu msaidizi wa Polisi Lucy Teesa kutoka Makao Makuu ya kikosi cha Kuzuia wizi wa
Mifugo STPU amewaomba wanaweka wenzake kushiriki vyema katika mapambano dhidi
uhalifu ambapo amewaomba kutoa taarifa za uhalifu na kujikitaa katika malezi bora ya Watoto
ili kujenga Jamii iliyostarabika.
Kwa upande wake Mkuu wa kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi Murieti Mrakibu msaidizi wa Polisi
ASP Tausi Mbalamwezi amewaomba wanawake wenzake kujiamini na kujituma katika
kutekeleza majukumu yao huku akiwaomba kuumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuliinua taifa kiuchumi.

Read More

Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi amezidi kuyafikia makundi mbalimbali kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi. Miongoni mwa kikundi kilichofikiwa na mkono wa kheri ni kikundi cha Mwanamke Shujaa cha Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ambacho kimechangiwa shilingi milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa mabanda ya kufugia mifugo mbalimbali yeye akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika Kiwilaya Tukuyu mjini lengo ni kupata 20m kufanikisha malengo. MAHUNDI ACHANGIA 5M KIKUNDI CHA MWANAMKE SHUJAA RUNGWE Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum…

Read More

#mbeyayetutv

Miaka 8 ya Jumuiya ya Maridhiano na Amani JMAT ilivyoadhimisha Wilayani Kyela.

Mkuu wa Wilaya ya Kyela Josephine Manase amesema Wilaya ya Kyela imeadhimisha Kitaifa Maridhiano Day kwa kuendesha ligi Maalumu ya Kombe la (Samia Maridhiano Cup)ambalo limefikia kilele kwa michuano ya soka.

DC Manase amesema michezo hiyo ya Samia Maridhiano Amani Cup limeacha ujumbe wa amani na ushirikiano kwa wakazi wa wilaya ya Kyela.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano ya Amani Tanzania JMAT Dkt Sheikh Alhad Mussa Salum amesema kombe hilo limechochea ushirikiano wa kijamii kwa kuwahusisha viongozi wa madhehebu ya dini zote.

Read More

Kampuni kubwa zinazojishughulisha na masuala ya utalii duniani zimevutiwa kuwekeza nchini Tanzania katika huduma za malazi, usafirishaji na utangazaji utalii. Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) katika Maonesho ya Utalii ya ITB yanayoendelea jijini Berlin Ujerumani. “Nimefurahi kukutana na kampuni kubwa ya TUI (TUI Group) yenye Makao Makuu nchini Ujerumani ambayo ina hoteli zaidi ya 400 duniani, meli za kitalii 16, mashirika ya ndege matano na zaidi Mashirika 1,200 ya usafiri” Mhe. Kairuki amesisitiza. Na Mwandishi Wetu-Berlin Kampuni kubwa zinazojishughulisha na masuala ya utalii duniani zimevutiwa kuwekeza nchini Tanzania katika huduma za malazi, usafirishaji…

Read More

Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi- Arusha.

Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha TPF-Net katika kuelekea siku ya wanawake Duniani leo wamefanya ibada maalumu kwa ajili ya kuwaombea Askari Polisi wanandoa waliofariki Dunia kwa ajali ya gari siku mbili baada ya kufunga ndoa.

Akiongea mara baada ya ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Theresia Jijini Arusha Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoani humo Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Happiness Temu amesema mtandao huo umekuwa na utaratibu wa kuyakumbuka makundi mbalimbali yenye uhitaji katika jamii ambapo kwa mwaka huu waliona ni vyema kuwakumbuka Askari waliofariki kwa ajali.

ASP Temu amebainisha kuwa wameamua kufanya Ibada hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwaombea marehemu hao ambao walikua wanafanya nao kazi Mkoani humo kabla kupatwa na umauti Disemba 20, 2022 ambapo pia katika ibada hiyo wamewaombea Watoto wawili ambao waliachwa na marehemu.

Nao baadhi ya askari wa mtaandao huo waliofanya kazi kwa Karibu na marehemu wamebainisha Pamoja na kuwaombea marehemu, pia wametumia ibada hiyo kumshukuru Mungu kwa kuendelea kuwalinda katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande wake Mrakibu wa Polisi SP Asia Matauka ambaye anafanya kazi katika Mkoa wa Kilimanjaro amesema mara baada kusikia juu ya uwepo wa ibada hiyo aliona ni vyema kuungana na mtaandao huo kuwaombea marehemu.

Askari waliofariki na kufanyiwa ibada leo ni Konstebo Noah Simfukwe na Agness Martin.

Read More

Mkurugenzi wa kampuni ya usambazaji mbolea ya Bens Patrick Mwalunenge ameahidi kutekeleza ahadi yake ya kutoa shilingi milioni kumi endapo Tanzania Prisons itazifunga timu za Simba na Yanga.

Akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari meneja wa Bens Israel Mwampondele baada ya Tanzania Prisons kufanikiwa kuifunga Simba mabao 2-1 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro jumatano machi 6,2024 Mwalunenge ameahidi kuikabidhi timu hiyo pindi itakaporejea Mbeya baada ya kumaliza michezo ya ugenini.

Mbali ya ahadi hiyo Mwalunenge ameahidi kumjengea nyumba mchezaji bora baada ya kutamatika ligi ya NBC.

Read More