Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- Ndipo akashinda Sh13 milioni kupitia betting
- WAZIRI ULEGA AAGIZA UPANUZI BARABARA YA TUNDUMA KWA HARAKA KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MALORI MPAKANI
- HIVI NDIVYO MWILI WA MAREHEMU JENISTA MHAGAMA ULIVYOWASILI NA KUPOKEWA SONGEA MKOANI RUVUMA
- MTARO ULIOFUKIWA MTAA WA LUMBILA IWAMBI MBEYA WAFURIKA MAJI YA MVUA NA KUIBUA KIZAAZAA KWA WANANCHI
- Mauzo yalianza kuongezeka, wateja wakawa wakudumu!
- Mtoto wa Jenista Mhagama Aibua Hisia Kali, Asema Mama Yake Hana Deni
- RAIS SAMIA KWA UCHUNGU MSIBANI – ”TUTALIMISI TABASAMU LAKE –
- MADEREVA BODABODA MKOANI IRINGA WALAANI VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI.
Author: Mbeya Yetu
Na Mwandishi Wetu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeandaa mafunzo maalumu kwa Mtandao wa Mabloga (TBN) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Mafunzo haya yatafanyika Jumatatu, Agosti 11, 2025, katika Makao Makuu ya TCRA. Kwa mujibu wa taarifa kutoka TCRA mafunzo hayo yana lengo la kuwaandaa mabloga na wanahabari kwa ujumla ili waweze kuripoti habari za uchaguzi kwa weledi na uadilifu. Mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wataalamu kutoka taasisi tofauti. Baadhi ya mada zitakazojadiliwa ni pamoja na Mwongozo wa Waandishi wa Habari katika Uandishi wa Habari za Uchaguzi, Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa za Mwaka 2020, na…
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for African Farmers Party (AAFP), Mhe. Kunje Ngombale Mwiru. Mgombea huyo wa AAFP aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Shum Juma Abdalla (kushoto) alichukua fomu hizo leo Agosti 9,2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. (Picha na INEC). Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs…
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mgombea huyo wa CCM alichukua fomu hizo leo Agosti 9,2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. Mgombea wa Kiti cha Rais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza wake Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi wakionesha mkoba wa fomu za kuomba kuteuliwa na…
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima akizungumza wakati akitangaza ratiba na orodha ya vyama ambavyo wagombea wake wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watafika katika Ofisi za Tume Njedengwa Jijini Dodoma kuchukua fomu za utezi kwaajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Kailima amesema hadi kufikia leo Agosti 08, 2025 vyama 14 vimeijulisha Tume ratiba ya wagombea wa vyama husika kuchukua fomu. Zoezi hilo litaanza Agosti 09 hadi 27 mwaka huu na vyama vingine vitakavyojitokeza vitapangiwa ratiba. ******* Na Mwandishi Wetu Tume Huru ya Taifa…
#Waipongeza kwa kuwafungulia barabara wakulima Dodoma Manaibu Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI wakiongozwa na Mhandisi Rogatus Mativila Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) Sospeter Mtwale – Naibu Katibu Mkuu (TAMISEMI)) na Prof. Tumaini Nagu – Naibu Katibu Mkuu (Afya) wametembea Banda la Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika kilele cha Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni, Jijini Dodoma. Makatibu Wakuu hao wamepatiwa maelezo mbalimbali kutoka kwa Wataalamu wa Wakala huo wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Bi. Catherine Sungura kuhusu majukumu, utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na mipango…
Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene, pamoja na mpiga picha wa zamani wa Rais, Ikulu, Fredrick Maro, wamekabidhiwa rasmi Vitambulisho vyao vya Uandishi wa Habari (Presscard) leo tarehe 07 Agosti 2025, baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa Sheria. Zoezi hilo limefanyika katika Ofisi za Bodi zilizopo Mtaa wa Jamhuri, jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula. Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi vitambulisho hivyo, Wakili Kipangula alibainisha kuwa Mwambene na Maro wamefuata utaratibu wa kisheria, ikiwa ni pamoja na kujisajili,…
