Author: Mbeya Yetu

Wananchi wa Jimbo la Uyole, Mkoani Mbeya, kwa moyo wa upendo na imani kubwa, wamemchukulia fomu ya kuwania tena Ubunge Dkt. Tulia Ackson @tulia.ackson kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2025. Hatua hiyo inaonesha wazi dhamira ya wananchi kuendelea kumuunga mkono kiongozi huyu mahiri ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa jimboni humo.

Wakizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, baadhi ya wakazi wa Uyole wamesisitiza kuwa Dkt. Tulia ni chaguo sahihi kutokana na utendaji wake uliotukuka, uwezo mkubwa wa kiuongozi na ushirikiano wake wa karibu na wananchi katika kutatua changamoto mbalimbali.

Kwa kauli moja, wananchi hao wameahidi kuendelea kumpigania hadi ushindi, wakiamini kuwa uongozi wake utaendeleza kasi ya maendeleo na kuimarisha ustawi wa wananchi wa Uyole.

Read More

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya waratibu, waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki wa Magereza kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyoanza leo Juni 22 -24, 2025 mkoani Dodoma. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya waratibu, waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki wa Magereza kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyoanza leo Juni 22 -24,…

Read More