Author: Mbeya Yetu

Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma Taifa, Ipyana Samson Njiku, leo Tarehe 25/08/2025 amechukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Uyole kupitia chama hicho.
Ipyana amesema hatua hiyo ni sehemu ya dhamira yake ya kuwatumikia wananchi wa Uyole kwa uadilifu, uwajibikaji na kusimamia maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Amesisitiza kuwa chama chake kimejipanga kutoa mbadala mpya wa kiuongozi unaolenga kuleta matumaini mapya kwa wananchi.

Read More

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini mkoani Mbeya, Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 25 Agosti 2025, amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya wananchi wa Jimbo jipya la Uyole katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Dkt. Tulia amechukua fomu hiyo katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) zilizopo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, huku akipokelewa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), viongozi wa ngazi mbalimbali pamoja na wafuasi wake waliokuwa na shauku kubwa ya kumuona akiendelea kulitumikia Taifa kupitia jimbo hilo jipya. Aidha, amewataka wananchi wa Uyole kuungana naye katika safari ya maendeleo,…

Read More

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Beno Malisa Agosti 22, 2025 amemkabidhi boti moja mpya PB.44 ULINZI Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga. Akikabidhi boti hiyo kwa Jeshi Mkoa wa Mbeya, Mhe Malisa amelitaka Jeshi hilo kulitumia vizuri boti hilo katika kuimarisha doria za ziwa nyasa Wilayani Kyela na kutokomeza uhalifu. nipe vichwa vitano vya habari Aidha, Mhe.Malisa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura kwa kutimiza ahadi ya kutoa boti kwa ajili ya kuimarisha ulinzi Ziwa Nyasa na kuahidi kuitunza na kuitumia vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa. Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga amesema kuwa Boti hiyo inakwenda kuimarisha ulinzi Ziwa Nyasa kupitia doria za pamoja za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, JWTZ, Uhamiaji na TRA. Ziwa nyasa ni miongoni mwa maziwa makuu nchini ambalo sehemu ya Ziwa hilo ni nchi jirani ya Malawi na Mkoa wa Njombe na Ruvuma hivyo uwepo wa Boti hiyo ni mikakati ya kuimarisha ulinzi na kudhibiti uhalifu wa majini.

Read More

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Askari Wanyama pori [TAWA] kutoka Mpanga Kipengele linamshikilia Frank Alon [49] mkazi wa Uyole – Nsalaga Jijini Mbeya kwa tuhuma za kupatikana na nyara za serikali meno nane [08] ya Tembo yenye uzito wa kilogram 31.6 bila kibali.

Mtuhumiwa alikamatwa Agosti 17, 2025 saa 9:00 alasiri Kijiji cha Nsonyanga kilichopo Kata ya Mahongole, Tarafa ya Ilongo, Wilaya ya Mbarali katika muendelezo wa Misako na Doria za pamoja zinazofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Askari Wanyama Pori [TAWA].

Mtuhumiwa alikuwa akisafirisha meno hayo ya Tembo kwa kutumia usafiri wa Pikipiki yenye namba za usajili MC 165 DDF aina ya TVS akiwa katika harakati za kutafuta mteja. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa ni mwindaji haramu katika hifadhi za Taifa.

Read More

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Maafisa wa Shirika la Umeme [TANESCO] Tawi la Mbeya linamshikilia Ikupa Mwakibibi [32] mjasilimali na mkazi wa Sae Jijini Mbeya kwa tuhuma za kuhujumu miundombinu ya Shirika la Umeme kwa kujiunganishia umeme kinyume na utaratibu wa shirika hilo.

Mtuhumiwa alikamatwa Agosti 18, 2025 saa 9:30 alasiri Mtaa wa Sae uliopo Kata ya Ilomba Jijini Mbeya katika oparesheni za pamoja za Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Shirika la Umeme [TANESCO] ambapo baada ya kupekuliwa katika nyumba yake mtuhumiwa alikutwa akiwa na mita za umeme 19, rimoti za TANESCO 45 pamoja na waya rola 25 vyote vikiwa ni mali ya shirika la TANESCO.

Read More