Author: Mbeya Yetu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa saba [09] kwa tuhuma za utapeli na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na WhatsApp. Watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti katika Misako inayofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya ambapo Agosti 18, 2025 saa 6:00 mchana huko Kitongoji na Kata ya Nsalala, Tarafa ya Usongwe, walikamatwa watuhumiwa 04 wanaojishughulisha na utapeli wa fedha kupitia mitandao ya Facebook na WhatsApp kwa kudanganya wanatafuta wafanyakazi wa kuuza Supermarket iitwayo Kajala iliyopo Jijini Dar es salaam.

Watuhumiwa waliokamatwa ni Nemia Japhet Njonga [23] fundi rangi, mkazi wa mwakapangala, Ombeni Asangalwisye Ambilikile [22] Bodaboda, mkazi wa Nsalala, Jacob Peter Hamis [23] fundi rangi, mkazi wa mwakapangala, Baraka Joniphat Mgala [22] Bodaboda, mkazi wa mtaa wa Ndola Mbalizi.

Watuhumiwa wamekuwa wakitengeneza link za kughushi kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na WhatsApp ambapo mtu anayeomba ajira hutumia kujiunga kwenye kundi hilo na kisha hutumiwa ujumbe unaomtaka kutuma CV yake na kumuomba mtume fedha za kujaziwa fomu na kulipia sare za kufanyia kazi. Watuhumiwa wamekutwa wakiwa na simu mbalimbali pamoja na laini za simu za mitandao mbalimbali zilizosajiliwa kwa majina ya watu tofauti ambazo hutumika kupokelea fedha na kufanyia mawasiliano

Read More

Mbeya, Agosti 2025 – Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mbeya imetangaza kufanikisha uokoaji wa zaidi ya shilingi milioni 47 na kuziwezesha Halmashauri kuongeza mapato ya ndani kwa zaidi ya shilingi milioni 200 kupitia ufuatiliaji na udhibiti wa mianya ya rushwa na upotevu wa fedha za umma. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mbeya, Maghela P. Ndimbo, mafanikio hayo yametokana na kazi za ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, uchambuzi wa mifumo ya ukusanyaji mapato, na kudhibiti matumizi yasiyo sahihi ya fedha katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2025. Miradi ya Maendeleo…

Read More

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imepokea vifaa tiba vya kisasa monitor 15 kwa lengo la kuboresha huduma za uangalizi kwa watoto wachanga. Vifaa hivi, vilivyotolewa na Madau wa Maendeleo GOAL 3, vinatarajiwa kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya kwa watoto wanaohitaji msaada wa haraka na wa kitaalamu.

Akikabidhi vifaa tiba hivyo Mwamvuwa Mika Meneja Mradi Tanzania amesema thamira ya Goal 3 ni hakikisha Watoto wachanga wananzaliwa katika mazingira mazuri na pia wanapata huduma ambayo ni bora.
“Kwa kipindi hiki tumefika hapa hospitali ya rufaa ya kanda Mbeya kwaajili ya kufunga Impala monitors kwenye kitengo cha NIKU ili kuweza kuwasaidia Watoto wachanga wanaozaliwa kabla ya muda. Ningependa pia kutoa shukrani zangu za dhati kwa Uongozi wa hospitali kwasababu tumeweza kushirikiana hadi kwa hatua hii tuliofika leo ambapo tumeshazifunga monitors 15 na zimeshaanza kutoa huduma kwa Watoto walio wodini na pia tutaendelea kushirikiana ili kuwafika Watoto wengine walio kwenye hospitali zingine ” – Mwamvuwa

Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Bi. Myriam Msalale amemshukuru Madau wa maendeleo GOAL 3 kwa kuichagua Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kufanya kazi nayo na kuvipatia vifaa tiba hivyo ambavyo vimekuja kwa wakati na vitatusaidia sana katika kuboresha huduma kwa watoto wachanga na kutoa wito kwa watumiaji wa vifaa tiba hivyo kuvitunza kwa uangalifu wa hali ya juu ili viweze kudumu kwa muda mrefu na kuwahudumia Watoto waliokuja kupata matibabu.
.

Nae Dkt.Rehema Marando Daktari Bingwa mbobezi wa watoto wachanga, amesema kuwa msaada huo umeleta manufaa makubwa kwa watoa huduma na Watoto ambapo vitawezesha kuboresha huduma na kuongeza ufanisi wa utoaji wa matibabu na uangalizi wa hali ya juu kwa Watoto wachanga.

Read More

Mgombea wa Kiti cha Rais kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha National Convention for Construction and Reform – Mageuzi (NCCR-MAGEUZI), Mhe. Haji Ambar Khamis akiwa na Mgombea Mwenza, Mhe. Dkt. Eveline Wilbard Munisi wakionesha begi la fomu za uteuzi baada ya kukabidhiwa na Tume leo Agosti 15,2025. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha National Convention for Construction…

Read More