Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- Nilichukiwa na Kila Mwanamume, Leo Wananipigania Kama Niko Thamani Ya Dhahabu
- Bwana Afichua Jinsi Wake Wawili Walivyopanga Kumnyang’anya Mali Zote Kimya Kimya
- Shitambala Awajibu Wanaosambaza Uvumi: “Mimi ni Mwanachama Mwaminifu wa CCM”
- Shitambala Atangaza Rasmi Kumuunga Mkono Mwalunenge na Rais Samia
- Nilipunguza Uzito Bila Mazoezi, Siri Ni Majani Haya Maalum
- Nilipigania Shamba La Urithi Kwa Miaka 10 Sasa Nimeibuka Mshindi na Familia Imenitazama Kwa Hofu
- WAWINDAJI PANYA WILAYA MOMBA WASAMBABISHIA HASARA MKULIMA WA MAHINDI MBOZI GUNIA 200 ZATEKETEA MOTO
- Mama Afumaniwa Akimroga Mwanawe Ili Abaki Nyumbani Asiolewe
Author: Mbeya Yetu
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Kasim Majaliwa Majaliwa tayari amewasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Songwe ulioko Mkoani Mbeya na Kupokelewa na Mwenyeji wake Cde: Juma Z. Homera Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwaajiri ya kushiriki Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani Leo Tarhe18 March 2024 ambalo Kitaifa linafanyika Jijini Mbeya katika Ukumbi wa Eden Highlands Hotel.
NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amemuagiza Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Rebman Ganshonga, kuhakikisha anapeleka huduma ya maji kwenye vitongoji ambavyo bado havina huduma ya maji. Mhandisi Mahundi ametoa maagizo hayo leo Machi 17, 2024 akiwa katika muendelezo wa ziara ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ya kukagua utekelezaji wa miradi ya Maji Mkoani Ruvuma Akiwa ziarani pia Mhandisi Mahundi ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji ili miradi ya maji iwe endelevu. *WANANCHI ELFU 9,659 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI MALUNGU NYASA* NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi…
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeitaka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kujidhatiti katika utangazaji utalii ili kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na Utalii nchini. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) ameyasema hayo leo Machi 17,2024 wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Ofisi za Makao Makuu ya TTB jijini Dar es Salaam . TTB YATAKIWA KUJIDHATITI UTANGAZAJI UTALII NCHINI Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeitaka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kujidhatiti katika utangazaji utalii ili kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na Utalii nchini. Mwenyekiti…
WANANCHI MBEYA WALIA KUVAMIWA NA TAZARA
Wakazi wa Iyunga,Ivumwe,ltuha,ltezi na Nsalaga Jijini Mbeya wameiomba Serikali kutolea ufafanuzi mgogoro wa ardhi baina yao na Shirika la Reli Tanzania na Zambia(TAZARA)baada ya Shirika hilo kuweka mawe(Bicons)katika maeneo yao sanjari na kuwataka wabomoe nyumba zao zinazodaiwa kuwepo mita hamsini ndani ya hifadhi ya reli kinyume na makubaliano.
Wananchi hao kwa nyakati tofauti wakiwa na nyaraka mbalimbali kuhusiana na mgogoro huo wamepaza sauti zao baada ya kugonga ukuta ofisi zote ikiwemo TAZARA na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya.
Maadhimisho ya wiki ya maji yameanza machi 16,2024 ambayo yatahitimishwa machi 22,2024 kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa Jijini Mbeya na Mbeya Vijijini. Akitoa taarifa ya maadhimisho hayo kwa Waandishi wa Habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Mkurugenzi wa uzalishaji maji na usambazaji maji safi na usafi wa Mazingira Mhandisi Barnabas Konga amesema Wizara ya Maji imekuwa ikiratibu maadhikisho hayo kila mwaka kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa namba 47. Konga ameitaja baadhi ya miradi inayotekelezwa ambapo katika kipindi cha miaka mitatu upatikanaji wa…
NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amemtaka Meneja wa RUWASA Mkoa wa Njombe Mhandisi. Sadick Chakka, kuhakikisha anasimamia wananchi ambao wapo jirani na chanzo cha maji cha Igongwi kilichopo Mkoani humo, wawe wa kwanza kupata huduma ya maji kabla haijafika maeneo mengine yaliyopangwa. Kadhalika ametoa maagizo kwamba mradi huo ukamilike kabla ya tarehe 30 Juni, 2024 ili wananchi waweze kupata huduma ya maji safi na salama. Mahundi ameyasema hayo leo Machi 15, 2024,akiwa Mkoani Njombe kwenye muendelezo wa ziara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji.…
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhishwa na matumizi ya fedha za mradi wa UVIKO-19 za kuboresha miundombinu ya utalii katika Msitu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi uliogharimu takribani shilingi milioni 579.1 Hayo yamesemwa leo Machi 16, 2024 na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Najma Giga walipofanya ziara ya kukagua miradi iliyotekelezwa na Wakala ya Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika msitu huo. “Kamati imeridhishwa na matumizi ya fedha za UVIKO-19 hasa katika ujenzi wa kituo cha taarifa za utalii, ukiliangalia lina thamani halisi ya…
Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso amekutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Chrysoula Zacharopoulou, Waziri wa Nchi-Maendeleo ya Uchumi (Secretary of State for Economic Development) wa Ufaransa. Akizungumza malengo na dhamira ya kutoa mualiko kwa Wizara ya Maji Tanzania, Mheshimiwa Chrysoula amesema Serikali ya Ufaransa inatambua na kuthamini jitihada za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika dhamira ya kuimarisha huduma ya Maji kwa wananchi na kwamba wanaamini hiki ni kipaumbele chake katika kipindi cha uongozi wake na kusisitiza kwamba katika kuunga mkono jitihada hizo serikali yake ya awamu ya sita Serikali ya Ufaransa imejidhatiti kuwekeza katika miradi…
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Timotheo Mnzava leo Machi 14, 2024, imetembelea miradi inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufungua utalii wa Malikale kwenye magofu ya Kisiwa cha Kilwa Kisiwani ikiwa ni juhudi mpya za kuongeza zao jipya la utalii huo.
“Tunaposema tunapongeza juhudi za Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kwa vitendo kama hivi. Hapa katika miaka hii mitatu Serikali yake imetoa fedha kuendeleza utalii wa malikale ikiwemo boti mpya ya kisasa ambayo watalii wanaweza kuona ndani ya maji, gati la kushuka abiria, jengo jipya la kufikia abiria na miundombinu mingine ambayo imechagiza idadi ya watalii kuongezeka hapa kutoka wastani wa 2900 hivi hadi 6,400. Haya ndio mafanikio yenye maono,” alisema Mhe. Mnzava.
Ziara hiyo pia walikuwepo Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki, Naibu wake, Mhe. Dunstan Kitandula, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi na watendaji waandamizi kutoka Idara za Wanyamapori, Malikale na Misitu.