Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kuopoa mwili wa mtu jinsi ya kiume daraja la mto Magege Mtaa wa Masewe Kata ya Ilemi Jijini Mbeya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka thelathini na nane hadi arobaini.Akitoa taarifa eneo la tukio Askari wa zamu Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Sajini Abdalah Sebombo amesema tukio limetokea majira ya saa mbili kasorobo asubuhi machi 30,2024.Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa wa Maswe Japhet Mahinya amesema alipata taarifa kutoka kwa mwananchi naye baada ya kufika eneo la tukio na kitoa taarifa Polisi,Polisi walipofika waliona mwili ukiwa korongo la mto hivyo ikawalazimu kuwasilana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kuopoa mwili wa mtu jinsi ya kiume daraja la mto Magege Mtaa wa Masewe Kata ya Ilemi Jijini Mbeya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka thelathini na nane hadi arobaini.
Akitoa taarifa eneo la tukio Askari wa zamu Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Sajini Abdalah Sebombo amesema tukio limetokea majira ya saa mbili kasorobo asubuhi machi 30,2024.
Aidha ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifacmapema kupitia namba ya dharura 114.
Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa wa Maswe Japhet Mahinya amesema alipata taarifa kutoka kwa mwananchi naye baada ya kufika eneo la tukio na kitoa taarifa Polisi,Polisi walipofika waliona mwili ukiwa korongo la mto hivyo ikawalazimu kuwasilana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Baada ya kufika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji walifanikiwa kuuopoa mwili huo na kuwataka wananchi wafanye utambuzi lakini hakuna aliyeweza kumtambua.
Wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari hasa katika kipindi hiki cha masika ambapo maji hujaa katika mito au visima ili kuepusha maafa.
Wito umetolewa kwa yeyote aliyepotelewa na ndugu yake afike Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya ajili ya utambuzi.