Maadhimisho ya wiki ya maji yameanza machi 16,2024 ambayo yatahitimishwa machi 22,2024 kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa Jijini Mbeya na Mbeya Vijijini.
Akitoa taarifa ya maadhimisho hayo kwa Waandishi wa Habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Mkurugenzi wa uzalishaji maji na usambazaji maji safi na usafi wa Mazingira Mhandisi Barnabas Konga amesema Wizara ya Maji imekuwa ikiratibu maadhikisho hayo kila mwaka kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa namba 47.
Konga ameitaja baadhi ya miradi inayotekelezwa ambapo katika kipindi cha miaka mitatu upatikanaji wa maji kwa Jiji la Mbeya na Mji wa Mbalizi ni lita milioni 38.5 kwa siku mahitaji yakiwa lita milioni 90 kwa siku.
Mhandisi Leonidas Deogratius Meneja mradi wa Mwasenkwa amesema mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 5.2 utanufaisha wananchi 42,000 na utazalisha lita milioni 2.6.Kwa upande wake Afisa Habari John Nkana amesema mpaka sasa ofisi yake imepokea maombi 620 ya wateja wanaohitaji kuunganishiwa maji na mpaka sasa wanazo dira 12,000.Naye Meneja Mradi wa Ilunga Uswege Mwaipopo amesema ukikamilika utagharimu shilingi bilioni 4.8 na kunufaisha wakazi wa Idugumbi,Iyombe,Itimba,Mbalizi,Nsalala,ltende,Sistila na lwambi ambapo mradi umefikia aslilimia 98.Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uhakika wa Maji kwa Amani na Utulivu”
Maadhimisho ya wiki ya maji yameanza machi 16,2024 ambayo yatahitimishwa machi 22,2024 kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa Jijini Mbeya na Mbeya Vijijini.
Akitoa taarifa ya maadhimisho hayo kwa Waandishi wa Habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Mkurugenzi wa uzalishaji maji na usambazaji maji safi na usafi wa Mazingira Mhandisi Barnabas Konga amesema Wizara ya Maji imekuwa ikiratibu maadhikisho hayo kila mwaka kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa namba 47.
Konga ameitaja baadhi ya miradi inayotekelezwa ambapo katika kipindi cha miaka mitatu upatikanaji wa maji kwa Jiji la Mbeya na Mji wa Mbalizi ni lita milioni 38.5 kwa siku mahitaji yakiwa lita milioni 90 kwa siku.
Baada ya maboresho Mamlaka inatekeleza miradi yenye thamani ya shilingi bilioni10 inayotoa lita milioni 66.5 kwa siku.
Aidha miradi iliyotekelezwa ni pamoja na mradi wa Mwashali uliogharimu shilingi milioni 400 ukihudumia watu 6,000,Mradi wa Nzovwe lsyesye umegharimu shilingi milioni 930 ukuhudumia wakazi 30,000.
Mradi mwingine ni wa UVIKO 19 wenye thamani ya shilingi 758 ukihudumia watu 55,000 ambapo mradi wa Shongo Mbalizi uliogharimu shilingi bilioni 3.345 ukihudukia watu 80,000.
Mradi mwingine ni pamoja na mradi wa Ilunga wenye thamani ya shilingi bilioni 4.8 utakaohudumia watu 110,000 ambapo miradi yote kwa pamoja inagharimu shilingi bilioni 10.
Konga amesema Mradi wa Kiwira utakaoghaimu shilingi bilioni 250 utamaliza kabisa changamoto ya maji Mkoani Mbeya.
Mhandisi Leonidas Deogratius Meneja mradi wa Mwasenkwa amesema mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 5.2 utanufaisha wananchi 42,000 na utazalisha lita milioni 2.6.
Kwa upande wake Afisa Habari John Nkana amesema mpaka sasa ofisi yake imepokea maombi 620 ya wateja wanaohitaji kuunganishiwa maji na mpaka sasa wanazo dira 12,000.
Pia ametoa onyo kwa watu wanaoharibu miundo mbinu ya maji kuwa yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheia.
Naye Meneja Mradi wa Ilunga Uswege Mwaipopo amesema ukikamilika utagharimu shilingi bilioni 4.8 na kunufaisha wakazi wa Idugumbi,Iyombe,Itimba,Mbalizi,Nsalala,ltende,Sistila na lwambi ambapo mradi umefikia aslilimia 98.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uhakika wa Maji kwa Amani na Utulivu”