Madiwani wa Viti Maalum Jiji la Mbeya na Mbeya Vijini wametembelea miradi miwili ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya.Akitoa taarifa mbele ya Madiwani hao Afisa Uhusiano Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya Neema Stanton amesema lengo la ziara hiyo ni kuielezea miradi mbalimbali inayotekelezwa ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Maji iliyoanza machi 16,2024 na kilele chake ni machi 22,2024.Aidha Afisa Uhusiano wa Mamlaka ameipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maji ukiwemo mradi mkubwa wa Kiwira utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 250.
Attu Msai Diwani wa Viti Maalum kwa niaba ya Madiwani ameipongeza Mamlaka kwa namna inavyoisimamia na kuitekeleza miradi mbalimbali.
Katika hatua nyingine Msai amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha maiaka mitatu”ameupiga mwingi”alisema Msai.
Wiki ya maadhimisho ya Wiki ya Maji mbali ya kutembelea miradi itakwenda pamoja na zoezi la kusafisha vyanzo vya maji na upandaji miti kwenye vyanzo vya maji.
Madiwani wa Viti Maalum Jiji la Mbeya na Mbeya Vijini wametembelea miradi miwili ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya.
Akitoa taarifa mbele ya Madiwani hao Afisa Uhusiano Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya Neema Stanton amesema lengo la ziara hiyo ni kuielezea miradi mbalimbali inayotekelezwa ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Maji iliyoanza machi 16,2024 na kilele chake ni machi 22,2024.
Miradi iliyotembelewa ni mradi wa llunga uliopo Mbeya vijini wenye thamani ya shilingi bilioni 4.8 utakaunufaisha wakazi Mbalizi na Iwambi Jijini Mbeya pia mradi wa Itagano Mwasen kwa uliogharimu shilingi bilioni 5.2 unaonufaisha wakazi wa Mwasenkwa,Ilemi na Iganzo.
Aidha Afisa Uhusiano wa Mamlaka ameipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maji ukiwemo mradi mkubwa wa Kiwira utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 250.
Katika hatua nyingine Stanton amesema wao ni watekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Kwa upande wake Attu Msai Diwani wa Viti Maalum kwa niaba ya Madiwani ameipongeza Mamlaka kwa namna inavyoisimamia na kuitekeleza miradi mbalimbali.
Katika hatua nyingine Msai amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha maiaka mitatu”ameupiga mwingi”alisema Msai.
Wiki ya maadhimisho ya Wiki ya Maji mbali ya kutembelea miradi itakwenda pamoja na zoezi la kusafisha vyanzo vya maji na upandaji miti kwenye vyanzo vya maji.