Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Eng Maryprisca Mahundi (Mb.) alikuwa mgeni rasmi katika Hafla ya siku ya Kimataifa ya Wasichana katika TEHAMA, 2024. Hafla hiyo ilikuwa imeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Hafla hiyo ilishirikisha wanafunzi wa kike kuanzia ngazi ya Awali, Msingi, Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu kutoka Tanzania bara, Unguja na Pemba.
Naibu Waziri Mahundi aliipongeza TCRA kwa kuhamasisha ushiriki wa Wasichana katika masuala ya TEHAMA kwa kuwa ni muhimu sana katika kipindi hiki ambapo nchi inaelekea katika Uchumi wa Kidijitali.
Aidha, Mhe Naibu Waziri Mahundi alisisitiza watoto wa kike kupenda masomo ya Sayansi na Uhandisi yaani STEM (Sayansi, Teknolojia, uhandisi na Hisabati) kwa kuwa ndiyo yatawasaidia kuweza kuwa Wanasayansi wazuri siku za baadae.