Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya, kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Serikali ya Ujerumani(GIZ), leo tarehe 12/03/2024, wamekabidhi Mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya usafi katika Kata ya Sinde na Shule ya Sekondari ya Sinde.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, mwakilishi wa GIZ Mbeya, Mhandisi Agnes Sigareti, amesema lengo la mradi huu ni kuboresha afya na usafi wa mazingira na kutokomeza magonjwa ya mlipuko katika Kata Sinde kwa kutumia teknolojia rahisi ya kutoa majitaka katika makazi yasiyo na mpangilio rasmi.Mradi huu umegharimu Shilingi milioni 400.6, umelenga maeneo makubwa mawili ambayo ni Uboreshaji wa miundombinu ya Usafi shuleni uliohusisha ujenzi wa matundu 16 ya vyoo vya watoto wa kike kwa kuzingatia mahitaji maalumu, uboreshaji wa vyoo 5 vya walimu, sehemu ya kunawia mikono, chomeo la taulo za kike.
Pia, GIZ imewezesha, ujenzi wa uzio wa sehemu za kuchotea maji (Africa Spring) na Mfumo wa usafirishaji wa majitaka Kata ya Sinde. Mradi huu umegharimu Shilingi milioni 400.6, umelenga maeneo makubwa mawili ambayo ni Uboreshaji wa miundombinu ya Usafi shuleni uliohusisha ujenzi wa matundu 16 ya vyoo vya watoto wa kike kwa kuzingatia mahitaji maalumu, uboreshaji wa vyoo 5 vya walimu, sehemu ya kunawia mikono, chomeo la taulo za kike.
Pia, GIZ imewezesha, ujenzi wa uzio wa sehemu za kuchotea maji (Africa Spring) na Mfumo wa usafirishaji wa majitaka Kata ya Sinde.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya, kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Serikali ya Ujerumani(GIZ), leo tarehe 12/03/2024, wamekabidhi Mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya usafi katika Kata ya Sinde na Shule ya Sekondari ya Sinde.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, mwakilishi wa GIZ Mbeya, Mhandisi Agnes Sigareti, amesema lengo la mradi huu ni kuboresha afya na usafi wa mazingira na kutokomeza magonjwa ya mlipuko katika Kata Sinde kwa kutumia teknolojia rahisi ya kutoa majitaka katika makazi yasiyo na mpangilio rasmi.
Mradi huu umegharimu Shilingi milioni 400.6, umelenga maeneo makubwa mawili ambayo ni Uboreshaji wa miundombinu ya Usafi shuleni uliohusisha ujenzi wa matundu 16 ya vyoo vya watoto wa kike kwa kuzingatia mahitaji maalumu, uboreshaji wa vyoo 5 vya walimu, sehemu ya kunawia mikono, chomeo la taulo za kike.
Pia, GIZ imewezesha, ujenzi wa uzio wa sehemu za kuchotea maji (Africa Spring) na Mfumo wa usafirishaji wa majitaka Kata ya Sinde.
Aidha, Mkurugenzi mtendaji wa Mbeya UWSA CPA. Gilbert Kayange, amewashukuru GIZ kwa kutoa fedha na kusimamia utekeleza wa mradi huu ambao unaenda kuwa ukombozi kwa jamii,pia amewaasa wananchi kuhakikisha miundombinu inatumika ipasavyo na kutunzwa kwa manufaa vya vizazi vijavyo.