Timu ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya ikiongozwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya CPA Gilbert Kayange inapambana usiku na mchana kurejesha huduma ya maji katika maeneo ya Nzovwe,lyunga,Viwandani,lnyala,lkuti,Iwambi,TAZARA,Kalone,Itende na Sistila baada ya miundombinu ya mabomba katika chanzo cha Haji Halewa Kata ya Swaya kusombwa na maji machi 6,2024.Akitoa taarifa eneo la chanzo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya CPA Gilbert Kayange amewatoa hofu wananchi kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Mamlaka yake. Awali Kayange amesema wamefanikiwa kurejesha huduma chanzo cha lyela baada ya miundombinu pia kuharibiwa na mvua zinazoendelea Jijini Mbeya. Aidha Kayange amesema mabomba katika chanzo cha Haji Halewa yamegharimu zaidi ya shilingi milioni milioni thelathini na mbili. Timu ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya ikiongozwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya CPA Gilbert Kayange inapambana usiku na mchana kurejesha huduma ya maji katika maeneo ya Nzovwe,lyunga,Viwandani,lnyala,lkuti,Iwambi,TAZARA,Kalone,Itende na Sistila baada ya miundombinu ya mabomba katika chanzo cha Haji Halewa Kata ya Swaya kusombwa na maji machi 6,2024.
Akitoa taarifa eneo la chanzo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya CPA Gilbert Kayange amewatoa hofu wananchi kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Mamlaka yake.
Awali Kayange amesema wamefanikiwa kurejesha huduma chanzo cha lyela baada ya miundombinu pia kuharibiwa na mvua zinazoendelea Jijini Mbeya.
Aidha Kayange amesema mabomba katika chanzo cha Haji Halewa yamegharimu zaidi ya shilingi milioni milioni thelathini na mbili.
Hata hivyo CPA Gilbert Kayange amesema kukamilisha kwa miradi ya Halinji na Itagano kumesaidia upatikanaji wa Maji katika Jiji la Mbeya na Mji wa Mbalizi kwa asilimia sitini na nane.