Meneja wa Wakala wa Barabara nchini(TANRODS)Mkoa wa Mbeya Mhandisi Masige Matari amesema miradi mbalimbali ya barabara inayotekelezwa Mkoani Mbeya katika uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nchi jirani.Masige ameyasema hayo katika mkutano wake na Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya huku akiitaja mitandao mbalimbali ya barabara za TANROADS ambazo inatekelezwa ni kuwa jumla ya kilometa 1,403.3 ambapo kati ya hizo kilometa 469.3 ni barabara za lami na kilometa 934 ni za changarawe. Ameitaja baadhi ya miradi ya barabara za lami kuwa ni pamoja mradi wa njia nne kuanzia Nsalaga-lfisi kilometa 29 unaogharimu shilingi bilioni 138.718.Barabara nyingine ni ya Ibanda-Kajunjumele-Kiwira na Itungi Port kilometa 32 unaogharimu shilingi bilioni 38.359,mradi mwingine ni Katumba-Mbambo-Tukuyu Bujesi -Mbambo kilometa 10 na Tukuyu-Mbambo kilometa 7 kwa gharama ya shilingi bilioni 21.307.Aidha Masige amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Dkt Samia Suluhu Hassan serikali imejenga kituo cha huduma ya pamoja mpakani Kasumulu(Tanzania/Malawi)kwa gharama ya ya shilingi bilioni 26.4 mrdi huo umefikia asilimia zaidi ya 90 na sasa uepunguza msongamano wa magari,mradi mwingine umehusisha ukarabati wa uwanja wa ndege jengo la abiria pia njia ya kuruka na kutua ndege sanjari na kuweka taa za kuongoza ndege kwa gharama ya shilingi bilioni 33.8 ambapo kwa sasa uwanja unafanya kazi kwa saa 24 hivyo umeongeza pato la serikali. Hata hivyo Mhandisi Masige Matari amesema serikali inatarajia kuanza ujenzi wa barabara ya lami lgawa-Tunduma kilometa 218 pamoja na Uyole-Songwe batabara ya mchepuko kilometa 48.9 ambapo ikikamilika mbali ya kupunguza msongamano itasaidia kupunguza ajali.
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini(TANRODS)Mkoa wa Mbeya Mhandisi Masige Matari amesema miradi mbalimbali ya barabara inayotekelezwa Mkoani Mbeya katika uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nchi jirani.
Masige ameyasema hayo katika mkutano wake na Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya huku akiitaja mitandao mbalimbali ya barabara za TANROADS ambazo inatekelezwa ni kuwa jumla ya kilometa 1,403.3 ambapo kati ya hizo kilometa 469.3 ni barabara za lami na kilometa 934 ni za changarawe.
Ameitaja baadhi ya miradi ya barabara za lami kuwa ni pamoja mradi wa njia nne kuanzia Nsalaga-lfisi kilometa 29 unaogharimu shilingi bilioni 138.718.
Barabara nyingine ni ya Ibanda-Kajunjumele-Kiwira na Itungi Port kilometa 32 unaogharimu shilingi bilioni 38.359,mradi mwingine ni Katumba-Mbambo-Tukuyu Bujesi -Mbambo kilometa 10 na Tukuyu-Mbambo kilometa 7 kwa gharama ya shilingi bilioni 21.307.
Aidha Masige amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Dkt Samia Suluhu Hassan serikali imejenga kituo cha huduma ya pamoja mpakani Kasumulu(Tanzania/Malawi)kwa gharama ya ya shilingi bilioni 26.4 mrdi huo umefikia asilimia zaidi ya 90 na sasa uepunguza msongamano wa magari,mradi mwingine umehusisha ukarabati wa uwanja wa ndege jengo la abiria pia njia ya kuruka na kutua ndege sanjari na kuweka taa za kuongoza ndege kwa gharama ya shilingi bilioni 33.8 ambapo kwa sasa uwanja unafanya kazi kwa saa 24 hivyo umeongeza pato la serikali.
Hata hivyo Mhandisi Masige Matari amesema serikali inatarajia kuanza ujenzi wa barabara ya lami lgawa-Tunduma kilometa 218 pamoja na Uyole-Songwe batabara ya mchepuko kilometa 48.9 ambapo ikikamilika mbali ya kupunguza msongamano itasaidia kupunguza ajali.
Mradi mwingine unaotarajiwa kutekelezwa ni mradi wa Katumba-Mbambo-Tukuyu sehemu ya Katumba-Lupaso kilometa 35.3 Mbaka-Kibaji wenye urefu wa kilometa 20.7
Masige amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan Mkoani Mbeya jumla ya fedha zilizopokelewa hadi mwezi machi,2024 ni kama ifuatavyo:-
(i)Fedha za matengenezo shilingi bilioni 32.089
(ii)Fedha za miradi ya maendeleo shilingi bilioni 124.923.
Miradi iliyokamilika mpaka sasa ni pamoja na barabara ya Chunya -Makongolosi yenye urefu wa kilometa 39 pamoja na mzani wa Matundasi kwa gharama ya shilingi bilioni 67 ambapo barabara hi imeongeza thamani ya mazao na madini ya dhahabu katika Wilaya ya Chuya,barabara nyingine ni ya Kikusya-lpinda-Matema yenye urefu wa kilomet 39.1 kwa gharama ya shilingi bilioni 63.3 barabara hii imekuwa sehemu ya utalii wa fukwe za Ziwa Nyasa na safu za milima ya Livingstone.
Kukamilika kwa mtandao wa barabara Mkoani Mbeya mbali ya kuongeza pato la serikali utafungua fursa za utalii kutokana na wageni watakaotumia,Barabara ya TANZAM,Uwanja wa Ndege wa Songwe,Bandari ya Itungi na Mpaka wa Kasumulu.