Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali watu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Miriam Mmbaga amefungua Kikao cha Baraza Dogo la Wafanyakazi Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kikao kilichofanyika Jijini Mbeya akiwataka wafanyakazi kufanya kazi kwa uadilifu na kufika kwa wakati eneo la tukio. Kamishina Utawala na Fedha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Semwanza amesema Jeshi la Zimamoto limeendelea kufanya maboresho mbalimbali pamoja na kutoa elimu kwa jamii ambapo serikali imewaongezea vifaa vya kukabiliana na matukio ya ajali kwa kuwapatia magari kumi na mbili ya Zimamoto ambayo yatagawiwa kwenye mikoa mbalimbali. Charo Mangare Kaimu Kamishina wa Opesheni ambaye amesema wamepokea pongezi na maelekezo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kuahidi kuyafanyia kazi. Maada zinazojadiliwa ni pamoja na kanuni mpya ya mikopo ya PSSSF,mfuko wa uwezeshaji-UTT,elimu juu ya huduma za NMB na utekelezaji wa mpango wa bajeti katika kipindi cha julai 2023 hadi februari 2024 na mwelekeo wa bajeti mwa mwaka 2024/2025.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali watu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Miriam Mmbaga amefungua Kikao cha Baraza Dogo la Wafanyakazi Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kikao kilichofanyika Jijini Mbeya akiwataka wafanyakazi kufanya kazi kwa uadilifu na kufika kwa wakati eneo la tukio.
Katika hotuba yake Mmbaga amewataka watumishi wa Zimamoto na Uokoaji kufanya kazi kwa eweledi na uadilifu ili kuongeza mapato ya serikali zaidi akiwataka kuendelea kutoa elimu kwa jamii sanjari na kufika kwa wakati kwenye matukio.
Naye Kamishina Utawala na Fedha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Semwanza amesema Jeshi la Zimamoto limeendelea kufanya maboresho mbalimbali pamoja na kutoa elimu kwa jamii ambapo serikali imewaongezea vifaa vya kukabiliana na matukio ya ajali kwa kuwapatia magari kumi na mbili ya Zimamoto ambayo yatagawiwa kwenye mikoa mbalimbali.
Maada zinazojadiliwa ni pamoja na kanuni mpya ya mikopo ya PSSSF,mfuko wa uwezeshaji-UTT,elimu juu ya huduma za NMB na utekelezaji wa mpango wa bajeti katika kipindi cha julai 2023 hadi februari 2024 na mwelekeo wa bajeti mwa mwaka 2024/2025.