Katibu Mkuu Wizara ya Maji Engineer Mwajuma Waziri ametembelea Ujenzi wa Mradi wa Maji kutoka chanzo Cha Mto Kiwira Mkoani Mbeya ambapo amewataka Wasimamizi wa Mradi huo kuongeza Kasi na kubainisha kuwa kwa hatua waliyoifikia ya Ujenzi hatarajii kuona Mvua inakuwa kikwazo katika Ukamilishwaji wa Mradi huo.
Eng: Waziri amewapa Maelekezo Mkandarasi na Washauri wake kufanya marekebisho ya baadhi ya Maeneo na amemtoa wasiwasi kuhusu Malipo yake Wizara na Serikali kwa Ujumla kutomuangusha Mkandarasi huyo ambaye anasimamia Ujenzi wa Banio kwenye Chanzo Cha Mto Kiwira na Tank la Maji lenye Ujazo wa Litre Million 117 ambalo linajengwa eneo la Forest.
“Nawapongeza wataalam wote wa Maji kutoka Mbeya Pamoja na BODI ya Maji ya MAmlaka ya Maji kwa Usimamizi Mzuri wa Mradi huu, Ukweli tuko hatua Nzuri Kikubwa Tuongeze Kasi ya Ujenzi ili tukamilishe kwa Wakati Wananchi wa Mbeya wapate huduma ya Maji ya Uhakika” Amesema Eng Waziri
Ameongeza kuwa “Mkandarasi natambua Kuwa unadai Fedha za Mradi lakini nikuhakikishie kuwa Sisi Wizara tutalimaliza Hilo muda Mchache Ujao Mifumo ikishaanza kufunguka tuu tunaanza na Hilo kwahiyo wewe Fanya Kazi kuhusu Malipo Usiwe na Shaka Kabisa.”
Mama Edina Mwaigomole ni M/kit wa Bodi ya Maji kawakaribisha Wawekezaji wa Viwanda kusogea Mkoani Mbeya kumwekeza kwakuwa Mradi huo utakapokamilika utatimiliza Mahitaji ya Wananchi na kubaki na Nyongeza ya Lita za Kutosha ambazo zitatumika katika Shughuli zingine za Uzalishaji Mali kwa Wawekezaji n.k.