Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Arif Abbas Manji leo Desemba 14, 2024 wamekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kampuni ya Jio Creative Labs jijini Mumbai nchini India ambayo ni moja ya kati ya makampuni makubwa ya matangazo nchini India.
Lengo la kikao hicho ni kujadiliana namna bora ya kuitangaza Tanzania katika Soko la India na Bara la Asia.
Moja kati ya majadiliano ni namna ya kutangaza mazao ya kipekee kama uhamaji na uzaaji wa pamoja wa nyumbu katika Hifadhi za Taifa za Serengeti na Ngorongoro pamoja na upekee wa Zanzibar katika urithi wa Mambo ya Kale na kuwa kituo bora cha fungate na harusi.