kuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z. Homera amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Mbeya kuhakikisha wanawapatia huduma Nzuri na za Uhakika(Chakula Malazi n.k) Madaktari Bingwa wa Samia waliofika Leo Mkoani Mbeya kwaajiri ya Kuanza Kambi Maalum ya Matibabu katika Hospitali za Halmashauri za Wilaya Mkoani humo.
Ameyasema hayo Leo Septemba 30 2024 wakati akiwapokea Madaktari hao Bingwa kupitia Mpango Kabambe Wenye Kauli mbiu ya Madaktari Bingwa wa Dkt: Samia tumekufikia Karibu tukuhudumie ambayo itaanza Septemba 30 hadi Oktoba 06 2024.
Katika Hotuba yake RC Homera amesema Mkoa wa Mbeya umepokea Jumla ya Madaktari 50 ambapo Kila Hospital ya Halmashauri itapokea Timu ya Madaktari Bingwa Sita na Muuguzi mbobezi Mmoja isipokuwa Halmashauri ya Mbeya Jiji ambayo itakuwa na Madaktari Bingwa Saba.
“Ndugu Washiriki Nimeambiwa Mpango huu una Malengo Makuu Matatu 01. Kutoa huduma za Kibingwa kwa Wagonjwa wa Idara ya Nje na Idara ya Ndani na Kufanya Upasuaji Watoto na Watoto wachanga, Afya ya Kinywa na Meno,Usingizi na ganzi na Migupa na Ajali kwa Wananchi wa Mbeya Mjini” Amesema Homera
Malengo mengine ni Kuwajengea Uwezo Watoa huduma katika Maeneo Yao ya Kazi ili Kuimarisha utambuzi, Matibabu, upasuaji na Rufaa kwa Wagonjwa ngazi ya Haospitali za Halmashauri na ya Mwisho ni Kuimarisha wodi Maalum za Watoto wachanga(NCU).
Aidha amebainisha kuwa katika Kampeni ya Awamu iliyopita Mkoa wa Mbeya uliwafikia Wagonjwa 2859 katika huduma Mbalimbali ikiwemo huduma za Magonjwa ya kinamama Magonjwa ya Ndani, walikuwa na uhitaji wa upasuaji, Watoto na Watoto wachanga na Usingizi na ganzi.
Jumla ya Watoa huduma 307 walinengewa Uwezo katika Maeneo Mbalimbali wanayotolea huduma na Jumla ya kiasi Cha Fedha 53,06,654 kiliweza kukusanywa katika Kipindi Cha Kampeni hiyo.
Katika hitimisho lake RC Homera amemshukuru Dkt: Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea Kutoa Kipaumbele kwenye Sekta ya Afya hususani kuwasogezea Wananchi wake huduma hizi za kibingwa kwenye Hospitali Zetu za Halmashauri ikiwa na Lengo kubwa la kuwafikia Wananchi wengi zaidi Wenye shida Mbalimbali za kiafya.