Wanafunzi wa shule mbalimbali mikoa ya Nyanda za juu Kusini wametakiwa kuunda klabu za Mazingira ili kuendelea kutunza vyanzo vya Maji kuepusha ukame.
Wito huo umetolewa na Tilisa Mwambungu Afisa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambapo wananchi Mikoa ya Nyanda za Juu wamejitokeza kwa wingi kutembelea Uwanja wa Maonesho John Mwakamgale hususani katika banda la Baraza la Taifa la usimamizi wa Mazingira(NEMC).
Tilisa Mwambungu ni Afisa Mazingira Kanda ya Nyanda za Juu anaeleza elimu wanayoitoa katika banda lao ambapo baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na Sekondari wametembelea banda lao na kujifunza pia udhibiti wa kelele maeneo ya makazii.
Baadhi ya washiriki waliotembelea banda hilo wamefurahishwa na huduma zinazotolewa wakiwemo wanafunzi wa shule ya msingi Scripture Union iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya.
Baraza la Taifa la usimamizi wa Mazingira(NEMC) limetilia mkazo kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira na hutumia maonesho mbalimbali kufikisha ujumbe kwa jamii.